Mtume wa Darja Muhammad (rehema na amani zimshukie yeye na Ahlulbayt wake watoharifu) anasema kuhusiana na Mwanafunzi atakafariki akiwa katika Harakati za kuitafuta Elimu ya Dini: “Itakapomjia mauti Mwanafunzi wa Elimu akiwa katika hali hii, hufa akiwa shahidi.” Hadithi hii inaonyesha utukufu wa elimu na cheo kikubwa alichopewa anayejitolea kwa dhati katika kuijua dini na kuitumikia jamii kwa mwanga wa Qur’ani na mafundisho Safi ya Ahlul-Bayt (a.s).

18 Novemba 2025 - 15:50

Kifo cha Mwanafunzi (Jabir Madua) wa Jamiatul Mustafa - Dar-es-salaam, Tanzania | Na Hadithi ya Mtume(saww) kuhusu Vifo vya Watafutaji wa Elimu +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Imenukuliwa katika vitabu vya Wanazuoni wa Kishia kuwa mwenye kufa akiwa katika njia ya kutafuta elimu, au akiwa amejishughulisha na kuyatafuta maarifa ya dini, basi hufa akiwa na daraja ya shahidi. Miongoni mwa riwaya hizo ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Mtume Mtukufu (rehema na amani zimshukie yeye na Ahlulbayt wake), kama ilivyokuja katika Bihar al-Anwar:

قال رسولُ اللهِ (صلى الله عليه وآله):

"إِذَا جَاءَ الْمَوْتُ لطَالِبِ الْعِلْمِ وَهُوَ عَلَى هٰذِهِ الْحَال، مَاتَ شَهِيدًا"


“Itakapomjia mauti Mwanafunzi wa Elimu akiwa katika hali hii, hufa akiwa shahidi.”
Hadithi hii inaonyesha utukufu wa elimu na cheo kikubwa alichopewa anayejitolea kwa dhati katika kuijua dini na kuitumikia jamii kwa mwanga wa Qur’ani na mafundisho ya Ahlulbayt (a.s).

Kifo cha Mwanafunzi (Jabir Madua) wa Jamiatul Mustafa - Dar-es-salaam, Tanzania | Na Hadithi ya Mtume(saww) kuhusu Vifo vya Watafutaji wa Elimu +Picha

Kwa moyo mzito tunamkumbuka ndugu yetu na kijana mwadilifu, marehemu Jaber Madua, mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa nchini Tanzania, ambaye jana ameitwa na Mola wake akiwa bado katika uwanja wa kutafuta elimu. Marehemu alikuwa mwanafunzi mwenye juhudi kubwa, mwenye nidhamu, tabia njema, na bidii katika kujifunza elimu za Qur’ani na Ahlulbayt (a.s). Alijulikana na walimu wake kwa utulivu, uchapakazi na uaminifu, na hakuchoka kujitolea kuwasaidia wenzake.

Tunamkadiria mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni miongoni mwa mashahidi wa elimu, kwa mujibu wa bishara ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w). Tunamuomba Mola Mwingi wa rehema amrehemu, amsamehe makosa yake, amjaalie makazi mema katika pepo za neema, amuunganishe na kundi la Muhammad na Aali Muhammad, na ampe ujira wa wanaotafuta elimu kwa ikhlasi na unyenyekevu.

Kifo cha Mwanafunzi (Jabir Madua) wa Jamiatul Mustafa - Dar-es-salaam, Tanzania | Na Hadithi ya Mtume(saww) kuhusu Vifo vya Watafutaji wa Elimu +Picha

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake tutarejea.

Your Comment

You are replying to: .
captcha