Utawala
-
Mafanikio mawili ya Yemen ndani ya siku moja; Mashambulizi ya Kimaonyesho dhidi ya Hodeidah yazimwa na kushindwa/Meli "Magic Seas" Yazamishwa Baharini
Yemen, imefanikiwa kuitwanga meli iliyokuwa ikielekea maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala haram wa Kizayuni, na kuizamisha baharini.
-
Leo tuko katika vita kamili -vya jumla- kati ya Imani na Ukafiri |Wito wa uhamasishaji wa Vyombo vya Habari na Ubainishaji Mzuri ili Kutetea Mapinduzi
Leo hii, ndio maana tunaona kila mtu ulimwenguni akifurahi kwamba Israeli inapigwa na Makombora ya Iran. Pia tunaona umoja wa kitaifa ndani ya nchi, ambapo kila mtu analaani hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi yetu, isipokuwa watu wachache wabaya na waliolaaniwa ambao hata majina yao hayaruhusiwi kutamkwa na kutajwa.
-
Iran yaidungua ndege isiyo na rubani ya Israel MQ-9 iliyotengenezwa na Marekani
Naibu afisa wa kisiasa na usalama wa gavana wa Ilam ametangaza kuwa, ndege ya kisasa isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni ilidunguliwa na mfumo shirikishi wa ulinzi katika anga ya mkoa huo.
-
Picha za Ismail Fikri, jasusi wa Mossad aliyenyongwa asubuhi ya leo
Alikubali kuwa kibaraka na jasusi wa Mossad kwa malipo ya vipande vya karatasi za Dola ili aliuze na kuliumiza Taifa, na leo hii amepata haki yake ya kikatiba anayoistahili. Na huu ndio mwisho wa watu waovu ulivyo.
-
Mkuu wa Shirika la ujasusi la IRGC na Naibu wake Waliuawa Shahidi
Walinzi wa Mapinduzi walitoa taarifa na kutangaza kuuawa Shahidi Mkuu wa upelelezi Mohammad Kazemi na naibu wake.
-
Naibu wa Vyombo vya Habari vya Harakati ya Nujaba ya Iraq katika mahojiano na ABNA:
"Mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran ni siri ya kushindwa kwa Netanyahu huko Gaza"
Dakta Hussein al-Moussawi amesema: Kufeli kwa fedheha kwa sera ya Netanyahu katika kupata ushindi wowote katika vita dhidi ya Ghaza, kushindwa kwake kudhibiti migogoro ya ndani na kujaribu kuukimbia utawala huo nje ya nchi ni sababu nyingine ya shambulio hilo dhidi ya Iran.
-
Uchokozi wa Israel: Rais wa Iran aitaka Iraq kulinda mipaka yake, anga
Picha ya mchanganyiko inawaonyesha Rais wa Iran Masoud Pezeshkian (Kulia) na Waziri Mkuu wa Iraq Muhammad Shayya al-Sudani.
-
Dkt. Pezeshkian katika Mkutano wa leo wa Baraza la Mawaziri:
Marekani bila shaka yoyote ina mchango wa moja kwa moja katika hujuma za hivi karibuni za utawala wa Kizayuni | Majibu yatakuwa ya maamuzi makali
Rais wa Iran amekosoa uungaji mkono wa Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi kwa vitendo vya jinai vya utawala wa Kizayuni na kusema: "Kama vile vikosi vyetu vya kijeshi hadi hivi sasa vimemendelea kutoa majibu yanayofaa na yenye nguvu, iwapo hatua za kiuadui za utawala wa Kizayuni zitaendelea, basi majibu yatakuwa ya maamuzi na makali zaidi."
-
Safari za ndege zimehairishwa hadi ilani nyingine/Shule, Misikiti, na njia za chini ya ardhi zitafunguliwa kwa umma saa 24 kwa siku kuanzia leo usiku
Msemaji wa Serikali amesema: "Hakuna shida katika kusafirisha bidhaa, dawa, chakula, na mahitaji ya watu, haswa mafuta."
-
Tamko la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) imesisitiza katika tamko lake kwamba: kuanzisha vita dhidi ya Iran ya Kiislamu ni sawa na kuvamia harem (makao matakatifu) ya Ahlul-Bayt (a.s). Katika hali hii, wanaharakati wote wa haki duniani, hasa mashirika na jumuiya zilizo chini ya mwavuli wa Ahlul-Bayt na wale wanaohusishwa na Jumuiya hii, wanaweza sasa kwa sauti kubwa kuliko wakati wowote kusema wazi kuwa utawala wa Kizayuni ni wa kigaidi na mvamizi. Aidha, taifa la Iran, likiwa limeungana zaidi na thabiti kuliko wakati wowote, litatoa jibu kali na la wazi kwa utawala huu wa kihalifu na muuaji wa watoto.
-
Mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza yaendelea wakati Waislamu wakiadhimisha Eid al-Adha huku ikinukia harufu ya damu
Sambamba na maadhimisho ya Sikukuu ya Eid al-Adha, Ukanda wa Gaza kwa mara nyingine umeshuhudia mashambulizi makali na ya umwagaji damu kutoka kwa jeshi la utawala wa Kizayuni.
-
Kuuawa kwa "Mohammad Ali Jamoul", Kamanda wa Kikosi cha Makombora cha Hezbullah katika Shambulio la Ndege Isiyo na Rubani la Utawala wa Kizayuni
Mohammad Ali Jamoul, Kamanda wa kikosi cha Makombora cha Harakati ya Hizbullah, ameuawa Kigaidi kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani (drone) lililofanywa na utawala haram wa Kizayuni (Israel). Shambulio hili linaonekana kuwa sehemu ya mfululizo wa mashambulizi ya Israel dhidi ya viongozi na miundombinu ya Hizbullah.
-
Hatua mpya katika kuhalalisha uhusiano wa kawaida; Mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Imarati (UAE ) na utawala haram wa Kizayuni
Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE Abdullah Bin Zayed amejadili uhusiano wa pande mbili katika mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kizayuni Gideon Sa'er huko Abu Dhabi. Katika kikao hicho amesisitiza juhudi za kidiplomasia za kufikia usitishaji vita huko Ghaza, lakini mkutano huu ulifanyika katika hali ambayo utawala wa Kizayuni unaendelea kuua na kufanya mauaji ya kimbari huko Ghaza.