Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Guinea-Bissau imeingia katika kipindi kipya cha sintofahamu ya kisiasa baada ya kuripotiwa kwamba Rais wa nchi hiyo, Umaro Sissoco Embaló, amepinduliwa na kutekwa na maafisa wa jeshi kufuatia mfululizo wa milio mizito ya risasi iliyodumu kwa zaidi ya siku tatu katika mji mkuu, Bissau.

Tukio la Kukamatwa kwa Rais
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la BBC, Rais Umaro alikamatwa na maafisa wa kijeshi na kwa sasa yuko chini ya ulinzi mkali. Tukio hilo limetokea wakati taifa likiwa bado katika hali ya msisimko wa kusubiri matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili iliyopita.
Katika hatua iliyowashtua wengi, Rais Sissoco alipiga simu kwa kituo cha televisheni cha France 24 akiwa na sauti ya kutetemeka, akisema: “Nimewekwa chini ya ulinzi, nimeondolewa madarakani…”
Kabala ya kuendelea, simu yake ilikatika ghafla, jambo lililoibua maswali kuhusu hali yake ya usalama.
Jeshi Latangaza Kuchukua Madarasa ya Utawala
Baada ya sintofahamu hiyo, Brigedia Jenerali Denis N’Canha, Mkuu wa Brigedi ya Kijeshi mjini Bissau, alitokea katika televisheni ya taifa na kutangaza rasmi kwamba jeshi limechukua madaraka ya nchi.
Katika hotuba yake, Jenerali N’Canha alieleza kuwa:
- Kikosi chote cha ulinzi wa Rais kimetiwa mbaroni
- Mawaziri kadhaa wamekamatwa
- Matokeo ya awali ya uchaguzi yamefutwa
- Mipaka ya nchi yote imefungwa
Amesisitiza kuwa jeshi limechukua hatua hiyo “kwa maslahi ya taifa” na ameziomba raia kubaki watulivu.
Uchaguzi Wenye Utata
Guinea-Bissau ilikuwa ikisubiri tangazo rasmi la matokeo ya uchaguzi wa urais. Matokeo ya awali yalikuwa yakimpa Rais Umaro ushindi wa zaidi ya 90%, jambo lililozua maswali kutoka kwa wadau wa siasa.
Jenerali N’Canha amesema wazi kwamba uchaguzi huo ulikuwa na:
- Udadanganyifu mkubwa
- Shinikizo kwa Tume ya Uchaguzi
- Kubanduliwa kwa mgombea mkuu wa upinzani Fernando Dias ili kumpa Rais Umaro nafasi ya ushindi rahisi
Hatua za Mpito Zatangazwa
Jeshi limetangaza kwamba:
- Litaunda serikali ya mpito
- Litaongoza nchi kwa muda mfupi
- Litaandaa uchaguzi huru, wa haki na wenye uwazi
Wananchi wamehimizwa kuendelea na shughuli zao kwa utulivu huku jeshi likiahidi kulinda amani na kuhakikisha hakuna machafuko zaidi.

Your Comment