21 Juni 2026 - 08:40
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi la Iran Latangaza Kufungwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz

Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC Navy) limetangaza kuwa Mlango wa Bahari wa Hormuz umefungwa kwa meli zote na kuonya kuwa chombo chochote kitakachoukaribia kitakuwa kinahatarisha usalama wake.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC Navy) limetangaza kufungwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz kwa meli zote, likionya kuwa chombo chochote kitakachoukaribia kitakuwa katika hatari ya kiusalama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, taarifa iliyotolewa na Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi hilo imesema uamuzi huo umechukuliwa kutokana na kile ilichokitaja kuwa ni uhalifu wa utawala wa Kizayuni nchini Lebanon pamoja na madai ya ukiukwaji wa ahadi za usitishaji mapigano na Marekani.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mlango wa Bahari wa Hormuz umefungwa kwa meli zote hadi itakapotolewa taarifa nyingine, huku ikizitaka meli kutoukaribia, ikisisitiza kwamba usalama wa vyombo hivyo unaweza kuwa hatarini iwapo vitapuuzia onyo hilo.

Hormuz ni mojawapo ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta na gesi, hivyo hatua yoyote inayohusu njia hiyo huwa na athari kubwa kwa usafiri wa baharini na masoko ya nishati duniani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha