18 Agosti 2025 - 11:41
Ushindi wa 2–1 wa Wanafunzi wa Al-Mustafa(s) - Dar-es-Salaam: Michezo, Umoja, na Maendeleo ya Kielimu kwa Pamoja

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jumapili, 17 Agosti 2025 – Katika mechi ya kirafiki ya kusisimua iliyochezwa kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuhimiza afya ya mwili, wanafunzi wa Chuo cha Al-Mustafa (S) Jijini Dar-es-Salam - Tanzania, waliibuka washindi kwa kuifunga timu ya Mbezi Beach kwa mabao 2 kwa 1.

Ushindi wa 2–1 wa Wanafunzi wa Al-Mustafa(s) - Dar-es-Salaam: Michezo, Umoja, na Maendeleo ya Kielimu kwa Pamoja

Mchezo huo uliandaliwa kama sehemu ya juhudi za kukuza uhusiano kati ya taasisi za kielimu na jamii, huku pia ukiwa jukwaa la kukuza vipaji vya michezo miongoni mwa wanafunzi.

Licha ya ushindani mkali dhidi ya timu ya Mbezi Beach, vijana wa Al-Mustafa (s) walionyesha nidhamu, umoja, na juhudi za hali ya juu, hali iliyopelekea ushindi wao wa haki. Bao la ushindi lilifungwa katika dakika za mwisho za kipindi cha pili, na kuzua shangwe miongoni mwa mashabiki na wachezaji.

Msemaji wa timu ya wanafunzi alieleza kuwa ushindi huu ni kielelezo cha jinsi elimu na michezo vinaweza kuenda sambamba, alisema:

"Tunathamini si tu mafanikio ya kitaaluma, bali pia afya, mshikamano na roho ya ushirikiano. Ushindi huu ni wa kila mwanafunzi wa Al-Mustafa."

Ushindi wa 2–1 wa Wanafunzi wa Al-Mustafa(s) - Dar-es-Salaam: Michezo, Umoja, na Maendeleo ya Kielimu kwa Pamoja

Tukio hili linatarajiwa kuwa mwanzo wa mfululizo wa mashindano ya kirafiki kati ya taasisi mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha uhusiano baina ya elimu na jamii kwa ujumla.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha