Sheikh Maulid Hussein Kundya amesisitiza juu ya umuhimu wa kuisoma na kuifahamu Qur'an Tukufu, na kuwakumbusha Waumini kuizingatia kauli ya Mwenyezi Mungu ambapo amesema: "Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa".
Msikiti ni Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na ni Kituo cha kiroho, kijamii na kiutamaduni, na vile vile ni nyumba makhsusi kwa ajili ya Waislamu kufanya ibada mbalimbali ndani yake.