6 Januari 2026 - 16:30
Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba Afungua Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar Katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi +Picha

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefungua rasmi Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar iliyogharimu shilingi bilioni 6.1, katika maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, akisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika elimu kwa maendeleo ya taifa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 05, 2026, amefungua rasmi Skuli ya Sekondari Chukwani iliyopo Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba Afungua Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar Katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi +Picha

Skuli hiyo, ambayo ujenzi wake umegharimu jumla ya shilingi bilioni 6.1, imeanzishwa kwa lengo la kuwaandaa vijana wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na maadili mema, kwa kuunganisha kwa vitendo nadharia na mafunzo ya darasani, ili kukidhi mahitaji ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba Afungua Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar Katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi +Picha

Uanzishwaji wa skuli hiyo unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa Zanzibar, ikiwemo kuongeza fursa za elimu bora, kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuinua viwango vya elimu kwa watoto na vijana wa visiwani humo.

Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba Afungua Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar Katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi +Picha

Katika hafla hiyo, Dkt. Mwigulu Nchemba alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa juhudi na uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya elimu, akieleza kuwa hatua hiyo ni msingi imara wa maendeleo endelevu na ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho.

Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba Afungua Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar Katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi +Picha

Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba Afungua Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar Katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi +Picha

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha