Zanzibar
-
Tangazo la nafasi za Masomo ya Kuhifadhi Quran Tukufu - Jamiat Al-Mustafa - Zanzibar
Chuo cha Jamiat Al-Mustafa Zanzibar kimetangaza nafasi za masomo ya kuhifadhi Qur’an Tukufu pamoja na masomo ya Hawza kwa mwaka wa masomo 2027, huku usajili mpya ukitarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba 2026.
-
Mwenyekiti wa JMAT-Taifa Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum Aongoza Viongozi wa JMAT Kumfariji Rais Samia Suluhu Hassan Kufuatia Msiba wa Mumewe
JMAT Taifa imetoa pole na faraja kwa Rais Samia Suluhu Hassan na familia yake kufuatia kifo cha mumewe, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, huku viongozi hao wakisisitiza umuhimu wa amani na mshikamano katika kipindi hiki cha majonzi.
-
Sheikh Mkuu wa TIC Afanya Ziara Zanzibar Kutoa Pole kwa Rais Samia Kufuatia Msiba wa Mumewe
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, ameongoza ujumbe wa viongozi wa TIC kwenda Zanzibar kutoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mumewe, Marehemu Hafidh Ameir Hassan. Taarifa rasmi ya Ikulu inamtaja Hafidh Ameir kuwa mume wa Rais Samia.
-
Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba Afungua Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar Katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi +Picha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefungua rasmi Skuli ya Sekondari Chukwani Zanzibar iliyogharimu shilingi bilioni 6.1, katika maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, akisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika elimu kwa maendeleo ya taifa.
-
Rais Samia Afanya Mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na JKT Zanzibar
Mazungumzo hayo yamezingatia masuala mbalimbali ya usalama, ulinzi wa taifa, na maendeleo ya majeshi, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya majeshi na wananchi katika kuhakikisha amani na utulivu wa taifa.
-
Heshima na Unyenyekevu wa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa Wazee | Sala ya Ijumaa - Masjid Abdallah Rashid - Zanzibar
Rais Dkt. Mwinyi pia ameswali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa 'Abdallah Rashid', ikiwa ni hatua inayotekeleza utaratibu wake wa kawaida wa kusali katika Misikiti mbalimbali nchini, kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa kijamii na kudumisha mahusiano ya karibu kati ya Viongozi na Waumini.