11 Juni 2025 - 19:37
Dkt. Al-Had Mussa Salum - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) Azungumzia Mambo Matatu Muhimu kwa Mustakbali wa Taifa

JMAT imepanga kuendesha matembezi ya amani kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Makao Makuu ya Tanzania. Lengo ni kuleta Watanzania pamoja na kuhamasisha Amani na Maridhiano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, Tanzania – 10 Juni 2025 – Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), ametoa taarifa za kina kuhusu mambo matatu makuu yanayohusu mustakbali wa Taifa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Taarifa hii aliitoa katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya JMAT, Jijini Dar es Salaam.

Ufuatao ni Muhtasari wa Mambo Matatu Muhimu Yaliyobainishwa na Mwenyeki JMAT-TAIFA:

1. Matembezi ya Hiari ya Amani

JMAT imepanga kuendesha matembezi ya amani kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Makao Makuu ya Tanzania. Matembezi haya yatafanyika kwa miguu kwa umbali wa kilomita 452, kuanzia tarehe 9 Juni hadi 9 Julai 2025. Lengo ni kuleta Watanzania pamoja na kuhamasisha Amani na Maridhiano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu. Matembezi haya yatahusisha watu 300 na yatazinduliwa rasmi tarehe 19 Juni 2025 katika viwanja vya Mnazi mmoja kuanzia saa 9 asubuhi. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

2. Uzinduzi wa Kitabu cha 4R za Rais wa Jamhuri

JMAT itafanya tukio hili la uzinduzi wa Kitabu cha 4R za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambacho ni kitabu chenye ujumbe muhimu kwa Taifa zima la Tanzania.

3. Maonyesho ya Saba Saba

JMAT itaendelea kushiriki katika maonyesho ya Saba Saba, tukio la kila mwaka la kuonesha maendeleo na tamaduni za kitanzania, na mwaka huu wa 2025 itajitokeza kwa ushiriki wa ari na hali ya juu kama ilivyo kawaida.

Kwa ufafanuzi zaidi katika video inayoeleza kwa kina kuhusu mambo haya matatu, tembelea chaneli rasmi ya JMAT kwenye YouTube: JMAT ONLINE TV.

Mawasiliano:

Ofisi za Makao Makuu ya JMAT-Taifa.

Simu: [+255 689 366 666] Mratibu JMAT-Taifa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha