amani
-
Kiongozi wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan: Suluhisho la Kashmir ni Sharti la Amani ya Kudumu katika Ukanda huu
Kiongozi wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan ameeleza kuwa: > “Hadi pale ambapo suala la Kashmir halitatatuliwa kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa, kufanikisha amani ya kudumu katika ukanda huu kutabaki kuwa ni ndoto ya mchana (serabu) tu.”
-
Zanzibar | Rais Mwinyi Atoa Wito wa Kuendelea Kuliombea Taifa Amani
Alisema: “Kila ninapopata nafasi ya kuzungumza na Wananchi, nitaendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa amani na utulivu kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tunapata maendeleo.”
-
Mwanamke na Nusu - Mratibu JMAT-TAIFA na Balozi wa Amani Duniani wa Shirika la Amani la (IWPG), Bi.Fatima F.Kikkides Katika Mkutano wa JMAT - Dodoma
Mkutano huu ni katika muktadha wa kudumisha Amani na Utulivu wa Taifa letu la Tanzania na kulitakia Kheri na Baraka Taifa hili kwa ajili ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Wananchi.
-
Maneno Muhimu na ya Hekima ya Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum - kuhusu: Wanaoitwa Mitume na Manabii Tanzania, Udugu wa Watanzania, na Amani ya Tanzania
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania tutasimama na Serikali Daima katika kulinda na kudumisha Amani na Maridhiano ya nchi yetu kwa ajili ya Ustawi wa nchi yetu.
-
Kamanda wa Iran wa Vikosi vya Jeshi la Ardhini: Usalama kamili upo kwenye mipaka
Kudumisha utayari wa mapigano kwa ajili ya kuhifadhi na kutetea itikadi, watu, dini na nchi ni misheni ya kudumu ya vikosi vya kijeshi vya Iran, na vikosi vya jeshi la ardhini kamwe havipuuzi misheni hii takatifu hata kwa sekunde moja.
-
Maduro: Ninalaani vikali shambulio la kuchukiza na la aibu la Marekani dhidi ya Iran
Ninatangaza wazi na bayana mshikamano wangu kamili kwa watu imara na mashuhuri wa Iran, serikali yake, na watu wote ulimwenguni wanaopigania uhuru na amani.
-
Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tehran: Raia wa kawaida hawapaswi kuwa walengwa kamwe | Tunasimama bega kwa bega na Iran
Ujumbe huo unasisitiza kuwa: "Njia pekee ya kutoka katika mzozo huu ni diplomasia. Kupunguza mivutano na kuendeleza mazungumzo kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kwa kuzingatia roho ya Katiba ya Umoja wa Mataifa ndiyo njia salama zaidi ya kulinda maisha ya watu na kuhifadhi amani tunayohitaji."
-
Dkt. Al-Had Mussa Salum - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) Azungumzia Mambo Matatu Muhimu kwa Mustakbali wa Taifa
JMAT imepanga kuendesha matembezi ya amani kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Makao Makuu ya Tanzania. Lengo ni kuleta Watanzania pamoja na kuhamasisha Amani na Maridhiano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.
-
Idadi ya waliouawa Gaza imefikia watu 54,880 | Hali ni mbaya sana na watu wengi wanahitaji msaada wa kibinadamu
Hali ya Gaza inaendelea kuwa mbaya kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni. Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa ndani ya saa 24 zilizopita watu 108 wamepoteza maisha na wengine 393 wamejeruhiwa. Jumla ya waliofariki tangu kuanza kwa mashambulizi haya imezidi kufikia watu 54,000. Hali hii inahitaji mshikamano wa kimataifa ili kusitisha ukatili huu na kuanzisha mazungumzo ya amani.
-
Mahojiano Maalum ya Firdaus TV na Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum - Mwenyekiti JMAT-TAIFA Yaliyofanyika Katika Uwanja wa Michezo wa Mkwakwani, Tanga
Ni katika Kongamano la Qur'an Tukufu lililofanyiks Jijini Tanga. Tukio hilo liliimarisha misingi ya Amani, Mshikamano, Maridhiano, na Ushirikiano kati ya Watanzania, likiwa ni Jukwaa la kuendeleza Mafundisho ya Qur’an Tukufu yanayohimiza Utulivu na Maelewano ya Kijamii.
-
JMAT Yatoa Wito kwa Viongozi wa Dini Nchini Kenya wa Kushirikiana Katika Kuwaongoza Wananchi wao ili Kuheshimiana na Kutunza Mahusiano ya Amani
Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum: "Wakenya ni ndugu wa Watanzania, na mbali na uhusiano wa kijamii, ni ndugu wa damu. Tunatambua kuwa mizozo hii inahusu zaidi vijana wa Kenya, lakini ni muhimu kuwakumbusha kuwa heshima ni nguzo muhimu katika mahusiano ya mataifa. Tunaamini Kenya ina Viongozi wa Dini na Serikali wanaoweza kusaidia katika hili."
-
Ukabidhi wa Hiari wa Silaha Parachinar; Hatua Muhimu kuelekea Amani Endelevu
Baada ya utekelezaji wa Mkataba wa Amani wa Kohat, Waislamu wa madhehebu ya Shia katika wilaya ya Kurram, eneo la Parachinar nchini Pakistan, wamekabidhi silaha zao kwa hiari kwa wawakilishi wa jeshi na maafisa wa serikali ya Pakistan ili kuonesha nia yao ya kutafuta amani.
-
Siku ya Quds Duniani:
Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi Amani ya Dunia nzima
Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi na kuidumisha Amani ya Dunia nzima. Waislamu waishi kwa Amani, Wakristo waishi kwa Amani, na hata Mayahudi waishi kwa Amani, na mtu yeyote asionewe na kudhulumiwa popote pale alipo Duniani.
-
Ufafanuzi wa Kina na Maridhawa Juu ya Suala la Unabii Baina ya Waislamu na Wakristo
Sheikh Dk.Alhad Mussa Salum: "Wakristo wanaposema, au tunaposikia ikisemwa, au anapoitwa mtu kuwa ni Nabii au Nabii Mkuu, anaitwa hivyo kwa Istilahi ipi?! Hili ndio swali la msingi kujiuliza?. Anaitwa hivyo kwa Istilahi yetu sisi Waislamu au kwa istilahi yao hao ndugu zetu Wakristo?!. Kwa sababu katika suala la UNABII kila watu wana Istilahi zao".