Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a) -ABNA- Leo tarehe 23 Agosti 2025 – Jumamosi - Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya shahada ya Imam Hassan al-Mujtaba (a.s), kikao maalum cha kielimu kiliandaliwa na Madrasa ya Mabinti - Madrasa Hazrat Zainab (s.a) - ambapo wanafunzi walijadili kwa kina mambo mbalimbali kuhusiana na maisha na mchango wa Imam Hasan (a.s) katika historia ya Uislamu.
Katika kikao hicho, mada kuu iliyojadiliwa ilikuwa:
- Athari na maana ya Amani ya Imam Hasan (a.s) – wanafunzi walitathmini hali ya kisiasa ya zama zake na hekima iliyopelekea kufanya mapatano ya amani na Mu’awiya, pamoja na athari zake kwa kulinda dini ya Uislamu.
Pamoja na mjadala huo, wanafunzi walibainisha pia:
- Nafasi ya Imam Hasan (a.s) kama mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) na mrithi wa elimu na uongozi wa Ahlul-Bayt (a.s).
- Sifa zake za kipekee za kimaadili kama vile ukarimu, subira na msimamo wa kulinda haki, ambazo zinabaki kuwa urithi wa kudumu kwa Waislamu.
- Mafunzo kwa kizazi cha sasa, kwamba hekima ya Imam Hasan (a.s) katika kuchagua njia ya amani ni somo la kimaisha na kijamii, hasa katika kujenga mshikamano wa Kiislamu.
Washiriki wa kikao hicho walionyesha mshikamano na ari ya kuendelea kusoma zaidi kuhusu Ahlul-Bayt (a.s), na walihimizwa kuyafuata mafunzo ya Imam Hasan (a.s) katika maisha ya kila siku, ili kuimarisha imani na maadili ya Kiislamu.
Your Comment