Katika kikao hicho, mada kuu iliyojadiliwa ilikuwa:
Athari na maana ya Amani ya Imam Hasan (a.s) – wanafunzi walitathmini hali ya kisiasa ya zama zake na hekima iliyopelekea kufanya mapatano ya amani na Mu’awiya, pamoja na athari zake kwa kulinda dini ya Uislamu.
Tunawapongeza waalimu waliowafundisha wasichana hawa wa Kiislamu kwa bidii na uaminifu, na pia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Jamiatul Mustafa (s) - Tanzania, Hojjatul Wal Muslimin, Dr.Ali Taqavi aliyekuja na wazo hili muhimu na kulisimamia kwa hekima na juhudi kubwa.
Hafla hii imehudhuriwa na Madrasat kutoka Bilal Muslim – Kanda ya Pangani pamoja na baadhi ya Madrasa kutoka kwa ndugu zetu wa Kisuni. Hili ni jambo la faraja kubwa, linaloashiria mshikamano wa kijamii na wa kidini katika maeneo yetu.