4 Julai 2025 - 00:50
Mabanati wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni, Dar-es-salaam, Wapatiwa Vyeti vya (ICDL) Baada ya Kukamilisha Kozi hiyo ya Mafunzo ya Kompyuta

Tunawapongeza waalimu waliowafundisha wasichana hawa wa Kiislamu kwa bidii na uaminifu, na pia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Jamiatul Mustafa (s) - Tanzania, Hojjatul Wal Muslimin, Dr.Ali Taqavi aliyekuja na wazo hili muhimu na kulisimamia kwa hekima na juhudi kubwa.

Kwa Mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, (Tarehe 3 Julai, 2915) limefanyika zoezi la utolewaji wa Vyeti vya Kumaliza Mafunzo ya Kompyuta katika Kozi ya (ICDL), kwa Wanafunzi wa Kike (Mabanati) wa Madrasa Hazrat Zainab (sa), Kigamboni - Dar-es-salaam, waliokamilisha kwa mafanikio makubwa Kozi ya Ujuzi wa Kompyuta – ICDL katika Kitengo Makhsusi cha Wasichana.

Vyeti rasmi vya kuhitimu Kozi hiyo, vimekabidhiwa kwao kwa heshima kubwa kupitia Hafla Maalum iliyoandaliwa katika Mnasaba huo.

Hafla hiyo ililenga kutambua juhudi na bidii za Mabinti hawa katika kujifunza maarifa ya kisasa ya teknolojia, sambamba na elimu ya dini.

Tunawapongeza wanafunzi hawa kwa ushiriki wao kamili tangu mwanzo hadi mwisho wa kozi hii, hadi walipofanikiwa kupata vyeti hivi vya kitaalamu vya ujuzi wa kompyuta.

Pia, tunawapongeza waalimu waliowafundisha wasichana hawa wa Kiislamu kwa bidii na uaminifu, na pia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Jamiatul Mustafa (s) - Tanzania, Hojjatul Wal Muslimin, Dr.Ali Taqavi aliyekuja na wazo hili muhimu na kulisimamia kwa hekima na juhudi kubwa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu awalipe nyote kwa kheri hapa duniani na Akhera, na awape afya, nguvu na tawfiq katika kuhudumia Uislamu na Waislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha