Kigamboni
-
Somo la Qur’ani Tukufu Lafanyika Kila Wiki katika Madrasat Hazrat Zainab (s.a) Kigamboni
Programu ya kila wiki ya somo la Qur’ani Tukufu imefanyika katika Madrasat Hazrat Zainab (s.a.) Kigamboni, Dar es Salaam, chini ya ufundishaji wa Sheikh Muhammad Jaafar, kwa ushiriki wa wanafunzi wote wa madrasah hiyo.
-
Programu ya Asubuhi ya Kimaanawi Yaendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni
Wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, wameendelea na programu ya kila siku ya asubuhi kwa kusoma Qur’ani Tukufu, dua na ziyara mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha malezi ya kiroho, maadili ya Kiislamu na uhusiano wao na Qur’ani pamoja na Ahlul-Bayt (as).
-
Ibada ya Sala ya Ijumaa Yaadhimishwa na Kuhuishwa katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni - Dar-es-Salam
Ibada ya Sala ya Ijumaa ya wiki hii ilifanyika katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, ikiongozwa na Hujjatul-Islam Sheikh Ghawthi Nyambwa, ambaye katika Khutba zake alizungumzia masuala muhimu ya maisha ya kila siku pamoja na matukio ya mwezi wa Rabiul-Awwal, akisisitiza maisha, haiba na nafasi ya kijamii na kisiasa ya Hazrat Zainab (sa).
-
Wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (sa) Washiriki Usomaji wa Dua ya Nudba
Asubuhi ya Ijumaa, tarehe 25 Septemba 2026, wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, wamehuisha ibada ya kusoma Dua ya Nudba, ikiwa ni sehemu ya utamaduni wao wa kila Ijumaa wa kuimarisha ibada, maadili na mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as).
-
Mfululizo wa Vikao vya Qur’ani Waendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni, Dar es Salaam
Mfululizo wa vikao vya Qur’ani umeendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni – Dar es Salaam, chini ya uongozi na ufundishaji wa Sheikh Muhammad Jaafar. Vikao hivyo vinawalenga wanafunzi wa shule hiyo na vinazingatia kukuza uelewa wa Qur’ani kupitia elimu, kuhifadhi, usomaji, tafakuri na tafsiri ya aya za Qur’ani Tukufu. Kuendeleza programu hizi kunalenga kuwajengea wanafunzi uhusiano wa karibu na Qur’ani na kuwasaidia kuelewa na kutumia mafundisho yake katika maisha yao ya kila siku.
-
Dar es Salaam: Shule ya Hazrat Zainab (s.a) Yaendesha Mafunzo ya Lugha ya Kiajemi kwa Wanafunzi wa Hawza
Mafunzo ya lugha ya Kiajemi yaandaliwa kwa wanafunzi wa Shule ya Kiislamu ya Hazrat Zainab (s.a) Kigamboni, Dar es Salaam, kwa lengo la kuwaandaa wanaotarajia kuendelea na masomo ya Hawza na elimu ya juu nchini Iran.
-
Wanafunzi wa Hawzat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Wafanya Mtihani wa Historia ya Kiislamu, Wakijengewa Uelewa wa Urithi wa Ahlul-Bayt (as)
Mtihani wa somo la Historia ya Kiislamu wa Muhula wa Tano wawapa wanafunzi wa Hawzat Hazrat Zainab (sa) fursa ya kupima uelewa wao kuhusu historia ya Maimamu wa Ahlul-Bayt (as), ikiwemo Imam Ali al-Ridha (as), Imam Muhammad al-Jawad (as) na Imam Ali al-Hadi (as).Miongoni mwa maswali muhimu yaliyoonekana katika mtihani huo ni: Msimamo wa Imam Al-Hadi (as) kuhusu suala la kuumbwa kwa Qur’ani: Kupitia swali hili, tunajifunza msimamo wa Imam al-Hadi (as) kuhusu mjadala wa iwapo Qur’ani ni kiumbe au si kiumbe, pamoja na ushauri aliowapa wafuasi wake kuhusu mgogoro huo wa kuumbwa au kutokuumbwa kwa Quran. Mtihani wa aina hii una umuhimu mkubwa katika elimu ya Hawza, kwa sababu unawasaidia wanafunzi kuunganisha maarifa ya kihistoria na uelewa wa mafundisho, misimamo na changamoto zilizowakabili viongozi wa Ahlul-Bayt (as).
-
Hafla ya Ugawaji Zawadi kwa Washindi wa Mashindano ya Uandishi wa Muhtasari "Summary Writing" Yafanyika Kigamboni - Dar-es-salaam
Katika hafla iliyofanyika katika shule ya wasichana ya Kigamboni, washindi wa mashindano ya kuandika muhtasari kuhusu “Shahada ya Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (ra)” walikabidhiwa zawadi maalum katika mwendelezo wa masomo ya Qur’an chini ya usimamizi wa Bi. Fatma Ma‘suma, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha elimu, ubunifu na ushindani wenye tija kwa wanafunzi.
-
Taqwa na Umuhimu Wake | Ijumaa - Khutba na Sala ya Dhuhri katika Chuo cha Dini cha Wanafunzi wa Kike cha Hazrat Zainab (SA)- Kigamboni - Dar-es-salaam
Lengo Kuu la mada iliyowasilishwa ni: Kukuza roho ya ibada, kuimarisha umoja wa kijamii, na kuhimiza utamaduni wa Sala ya Ijumaa miongoni mwa wanafunzi wa dini
-
Hawzat ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni yaendelea kuhuisha Ibada ya Dua ya Nudba | Iliyojaa Mafunzo ya Subira, Imani na Mapenzi kwa Imam wa Zama (as)
Ibada hii hujenga umoja wa kiroho, maadili mema na moyo wa subira, na hivyo kufanya wiki kuanza kwa baraka na nuru ya dua.