26 Mei 2026 - 19:59
Hafla ya Ugawaji Zawadi kwa Washindi wa Mashindano ya Uandishi wa Muhtasari "Summary Writing" Yafanyika Kigamboni - Dar-es-salaam

Katika hafla iliyofanyika katika shule ya wasichana ya Kigamboni, washindi wa mashindano ya kuandika muhtasari kuhusu “Shahada ya Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (ra)” walikabidhiwa zawadi maalum katika mwendelezo wa masomo ya Qur’an chini ya usimamizi wa Bi. Fatma Ma‘suma, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha elimu, ubunifu na ushindani wenye tija kwa wanafunzi.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika mwendelezo wa masomo ya Qur’an yanayoendeshwa chini ya uongozi wa Bi. Fatma Ma‘suma, hafla maalum ya utoaji zawadi imefanyika katika shule ya wasichana ya Kigamboni kwa washindi wa mashindano ya kuandika muhtasari (summary writing).

Mashindano hayo yalikuwa yameandaliwa hapo awali na yalijikita katika mada ya “Shahada ya Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (ra)”, kwa lengo la kuwajengea wanafunzi uwezo wa uandishi, uelewa wa masuala ya Kiislamu pamoja na kuhamasisha usomaji na uchambuzi wa mada mbalimbali za kielimu na kiimani.

Katika hafla hiyo, baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri zaidi walitangazwa kuwa washindi na kukabidhiwa zawadi mbalimbali kama ishara ya kuthamini juhudi zao, bidii na mafanikio yao katika mashindano hayo.

Washiriki na walimu waliohudhuria hafla hiyo walieleza kufurahishwa na hatua hiyo, wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza programu za kielimu na Qur’ani zinazochochea vipaji na maadili mema kwa wanafunzi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha