Afrika
-
Ripoti ya Kina ya Mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Wanahabari wa AhlulBayt(as)kwa Ushiriki wa Wanahabari kutoka zaidi ya nchi 20 za Afrika +Picha na Video
Sambamba na Siku Kumi za Karama (The Ten Days of Karama), Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa 'Waandishi wa Habari wa Ahlul-Bayt (a.s)' umefanyika leo Alhamisi asubuhi, tarehe 1 Mei, 2025), katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) Mjini Qom, kwa Ushiriki wa Wanaharakati wa Habari na Wasomi kutoka Iran na Bara la Afrika.
-
Kuimarishwa kwa uhusiano wa kibiashara kati ya Iran na Afrika / Isfahan kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Afrika
Waziri wa Viwanda wa Mali, katika hafla ya kufunga Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Afrika, alisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji wa pamoja katika nyanja mbalimbali. Alieleza matumaini kwamba mkutano huu utasababisha mshikamano na maingiliano yenye tija kati ya pande hizo mbili, na akatambua kuwa sekta binafsi ina nafasi muhimu katika mchakato huu.
-
Afrika Katika Ramani ya Utalii wa Vyakula: Tanzania Yaongoza Jitihada
Tanzania inatazamiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la 2 la Umoja wa Mataifa la Elimu ya Utalii kwa Afrika Mwezi Aprili 2025, likileta pamoja wataalamu wa kimataifa ili kuangazia umuhimu wa utalii wa upishi katika kukuza uchumi na kukuza urithi wa vyakula mbalimbali Barani Afrika.
-
Samahat Sheikh Kadhim Abbas, Mudir wa Hawza za Bilal Muslim Tanga - Tanzania, amefanya ziara muhimu katika Hawza ya Imam Ali (a.s)
Sheikh Kadhim ametoa akitoa nasaha kwa nasaha kwa Wanafunzi amesema: "Wanafunzi wa Kidini wanapaswa kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo yao ili kuhakikisha wanayafikia malengo matukufu ya kuchuma Elimu na Maarifa ya Dini Tukufu ya Kiislamu".
-
Tunajifunza nini baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan?
Aliyekuwa akifanya Ibada za Usiku ndani ya Ramadhani na mwendo wake ukabadilika na tabia zake kuwa nzuri ndani ya Ramadhan, basi aendelee kuwa na tabia nzuri hivyo hivyo hata baada ya Ramadhan. Na hii ni sehemu ya wito na funzo zuri toka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).
-
Umuhimu wa Tabligh, Malengo na Mipango ya Jamiatul - Mustafa (S) nchini Tanzania
Jamiatul - Mustafa ipo tayari kusaidia na kushirikiana na wanaofanya kazi ya kufikisha Ujumbe, Elimu na Maarifa ya Ahlul_Bayt (a.s).
-
Mjukuu wa Nelson Mandela:
Shahidi Nasrallah ni kielelezo kwa watu wote walio huru duniani | Kuthamini uungaji mkono wa Iran ya Kiislamu kwa Palestina
Mandela alisema: Tunaheshimu kumbukumbu ya shujaa huyu na ushujaa wake na tunashukuru uongozi na wanachama wa Hezbollah kwa utetezi wao wa kijasiri wa Msikiti wa Al-Aqsa, watu wa Gaza na upinzani mzima wa Palestina.
-
Somalia na Sudan zimekataa ombi la kuwapa makazi Wapalestina wanaoishi Gaza
Mamlaka za nchi mbili, Somalia na Sudan, zimekataa katakata pendekezo na mpango wowote kuhusu uhamisho wa Wapalestina wanaoishi Gaza hadi katika eneo la nchi hizi za Kiafrika.