6 Mei 2025 - 17:47
Mwanamume Shujaa Kazini | Burkina Faso Yavunja Rekodi Katika Uzalishaji wa Vitunguu!

Burkina Faso sasa imeizidi Senegal katika uzalishaji wa vitunguu na kuwa nchi ya tatu kwa uzalishaji mkubwa wa vitunguu katika eneo la Afrika Magharibi.Mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi bora wa Rais Ibrahim Traoré, ambaye ameweka mkazo katika kuimarisha sekta ya kilimo na kuinua maisha ya wakulima wa kawaida.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Burkina Faso (BF) imeonyesha mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo, hasa kwenye uzalishaji wa vitunguu, na sasa imeizidi Senegal na kuwa mzalishaji wa tatu kwa ukubwa wa vitunguu Afrika Magharibi. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, Burkina Faso imeweza kuzalisha zaidi ya tani 400,000 za vitunguu, hatua inayoiweka karibu kufikia nafasi ya tisa kwa uzalishaji wa vitunguu barani Afrika.

Mwanamume Shujaa Kazini | Burkina Faso Yavunja Rekodi Katika Uzalishaji wa Vitunguu!

Aidha, nchi hiyo imejipatia umaarufu pia katika biashara ya nje ya zao hilo, kwa kuwa mzalishaji na msafirishaji wa pili kwa ukubwa wa vitunguu katika kanda, nyuma ya Niger pekee.

Maendeleo haya yanaashiria uwezo mkubwa wa kilimo cha Burkina Faso na juhudi za wakulima wake, sambamba na sera bora zinazowezesha kilimo chenye tija.

Mwanamume Shujaa Kazini | Burkina Faso Yavunja Rekodi Katika Uzalishaji wa Vitunguu!

Mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi bora wa Rais Ibrahim Traoré, ambaye ameweka mkazo katika kuimarisha sekta ya kilimo na kuinua maisha ya wakulima wa kawaida.

Mwanamume Shujaa Kazini | Burkina Faso Yavunja Rekodi Katika Uzalishaji wa Vitunguu!

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha