Niger
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso: Iran imekuwa mfano wa kipekee wa heshima na uhuru
Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Karamoko Jean Marie Traoré, amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa mfano wa kipekee wa heshima, uhuru na ustahimilivu, akipongeza msimamo thabiti wa wananchi wa Iran katika kukabiliana na vitisho na mashinikizo visivyo halali.
-
Burkina Faso, Mali na Niger Zazindua Operesheni ya Pamoja ya Kijeshi Dhidi ya Makundi ya Kijihadi
Kiongozi wa mpito wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré, ametangaza kuanza kwa hatua mpya za kijeshi katika eneo la Sahel baada ya nchi yake, kwa kushirikiana na Mali na Niger, kuzindua operesheni ya pamoja inayolenga kukabiliana na makundi ya kijihadi yanayohusishwa na Al-Qaeda na ISIS. Hatua hiyo inakuja katika muktadha wa kuimarishwa kwa muungano wa kijeshi wa nchi hizo tatu, huku zikisisitiza mshikamano wa kiusalama na mwelekeo mpya wa ushirikiano wa kikanda kufuatia kujiondoa kwao katika ECOWAS na kuvunja ushirikiano wa awali na Ufaransa na Marekani.
-
Kwa mwaka wa tatu mfululizo; Sudan yaongoza orodha ya migogoro ya kibinadamu duniani
Sudan kwa mwaka wa tatu mfululizo imeorodheshwa juu kabisa katika orodha ya migogoro ya kibinadamu duniani.Nchi nyingine zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo ni pamoja na: Myanmar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mali, Burkina Faso, Lebanon, Afghanistan, Cameroon, Chad, Colombia, Niger, Nigeria, Somalia, Syria, Ukraine na Yemen.