Rais Ibrahim Traoré, akizungumza katika mahojiano ya televisheni ya kitaifa, alithibitisha tukio hilo na kusema kwa maneno makali: “Kama kuna daktari, mwalimu, au mfanyabiashara anayehisi anajua zaidi kuhusu vita kuliko wanajeshi wetu, basi ni bora naye achangie kwa vitendo - aende vitani.”
Burkina Faso sasa imeizidi Senegal katika uzalishaji wa vitunguu na kuwa nchi ya tatu kwa uzalishaji mkubwa wa vitunguu katika eneo la Afrika Magharibi.Mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi bora wa Rais Ibrahim Traoré, ambaye ameweka mkazo katika kuimarisha sekta ya kilimo na kuinua maisha ya wakulima wa kawaida.