Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Leo Tarehe 3 Mei 2025, Balozi wa Iran nchini Kenya, Dkt. Ali Gholampour, ameonyesha nia ya kuimarisha ushirikiano wa michezo kati ya Iran na Kenya.
Akizungumza katika kipindi cha Sports Extravaganza kinachorushwa na TV47 na kuendeshwa na Tony Kwalanda, Dkt. Gholampour alisema kuwa michezo ni daraja muhimu la kuunganisha mataifa na jamii.
Katika mahojiano hayo, walijadili michezo mbalimbali ikiwemo kandanda, voliboli, kuinua vitu vizito, mieleka, pamoja na mchezo wa kitamaduni wa Iran unaojulikana kama Zurkhaneh. Balozi huyo alibainisha kuwa kuna fursa nyingi za ushirikiano kupitia mafunzo ya pamoja, mashindano ya kimataifa, na kubadilishana wataalamu wa michezo.
Dkt. Gholampour alisisitiza kuwa uhusiano wa kidiplomasia unaweza kuimarishwa zaidi kupitia sekta ya michezo, huku akiwataka wadau wa michezo kutoka Kenya kushirikiana na wenzao kutoka Iran katika kuinua viwango vya michezo mbalimbali.
Your Comment