3 Juni 2025 - 16:02
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (A) amewasili nchini Côte d'Ivoire na kukutana na Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire (Ivory Coast)

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (A) alikutana na Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire mara tu alipowasili nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (AS) -ABNA- Ayatollah Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS), alisafiri kwenda Côte d'Ivoire (Ivory Coast), nchi iliyopo upande wa Afrika Magharibi, kwa mwaliko wa viongozi wa kidini wa Côte d'Ivoire (Ivory Coast).

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) alipowasili uwanja wa ndege wa Côte d'Ivoire, alifanya mkutano mfupi na Bogere Mambe, Waziri wa nchi hiyo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (A) amewasili nchini Côte d'Ivoire na kukutana na Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire (Ivory Coast)

Mkutano wa Ayatollah Ramadhani na Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire

Katika mkutano huu, Amir Hossein Nikbin, Balozi wa Iran nchini Côte d'Ivoire, alifafanua malengo ya safari ya Ayatollah Ramezani katika nchi hiyo kwa Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire.

Inafahamika kwamba mikutano na wanazuoni, wataalamu, wasomi na vijana wa Côte d'Ivoire ni mojawapo ya mipango ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS) katika ziara yake nchini humo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha