Waziri
-
Waziri wa India: Qur’ani ni kwa Wanadamu Wote; Uislamu Unasisitiza Ubinadamu
Waziri wa Elimu ya Juu wa Jimbo la Karnataka, Basavaraj Rayareddy, ameuelezea Uislamu kuwa dini yenye mafundisho yanayosisitiza ubinadamu na kusema kuwa Qur’ani si kwa Waislamu pekee, bali kila mtu anaweza kuisoma. Pia ameeleza nia yake ya kutembelea Makka na kufanya ibada ya Hija.
-
Nchi za Ghuba ya Uajemi: Shinikizo la Kiuchumi la Marekani Dhidi ya Iran Si Uhalisia
Ripoti ya Ra’y al-Youm, ikinukuu vyanzo vya kidiplomasia vya Magharibi, inasema baadhi ya nchi za Ghuba zimeieleza Marekani kuwa mpango wa kuongeza shinikizo la kiuchumi dhidi ya Iran unaweza kuwa na athari kubwa za kiusalama na kiuchumi kwa nchi jirani.
-
Araghchi amjibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa: “Acheni machozi ya kinafiki”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amemjibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noël Barrot, akimkosoa kwa kutoa madai kuhusu haki za binadamu nchini Iran huku, kwa mujibu wa Araghchi, Ufaransa ikiwa kimya kuhusu mauaji ya wanafunzi wa Iran katika shambulio la Marekani. Pia alikumbusha historia ya ukoloni wa Ufaransa nchini Algeria na madai kuhusu idadi kubwa ya Waalgeria waliouawa wakati wa vita vya uhuru.
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Marekani Haiwezi Kujitenga na Wajibu Wake Katika Jinai za Kivita
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa, Kazem Gharibabadi, amesema matukio yaliyotokea katika miji ya Minab na Lamerd, kusini mwa Iran, yalikuwa jinai za wazi za kivita, na si makosa ya kiutendaji.
-
Ubalozi wa Iran: Uhalifu wa Vita wa Marekani Haufichiki kwa Maonesho ya Hollywood
Ubalozi wa Iran mjini London wakumbusha kuuawa kwa wanafunzi wa kike 168 katika shambulio la Marekani dhidi ya shule ya msingi ya “Shajarat al-Tayyiba” mjini Minab.
-
Waziri wa Sayansi wa Iran Aelekea Riyadh Kushiriki Mkutano wa UNESCO Kuhusu Akili Bandia
Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran, Hossein Simaei, ameondoka Tehran kuelekea Riyadh akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu kwa ajili ya kushiriki mkutano wa UNESCO kuhusu akili bandia (AI).
-
Araghchi na Mwenzake wa Uturuki Wafanya Mazungumzo ya Simu Kuhusu Kuzuia Kuenea kwa Mgogoro Katika Eneo
Iran na Uturuki zasisitiza umuhimu wa kuzuia kuongezeka kwa mvutano na kupanuka kwa wigo wa mgogoro wa kikanda, huku zikisisitiza kuendelea kwa mashauriano na juhudi za kidiplomasia.
-
Araghchi: Raia wa Marekani Hawapaswi Kulipia Gharama za Vita vya Utawala wa Kizayuni
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema wananchi wa Marekani hawapaswi kubeba gharama za vita vya utawala wa Kizayuni, akirejea kauli ya Kaimu Waziri wa Jeshi la Wanamaji la Marekani kuhusu kuvunjwa kwa makao ya majeshi ya Marekani nchini Bahrain.
-
Balozi wa Iran katika OIC Akutana na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi
Balozi wa Iran katika Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amempa Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi taarifa kuhusu shughuli za Iran ndani ya OIC na kujadili njia za kuimarisha hatua za pamoja za nchi za Kiislamu dhidi ya mashambulizi ya Israel Palestina na Lebanon.
-
Araghchi Aitaka Marekani Kuheshimu Ahadi Zake Katika Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kurejea kwa Marekani katika kutekeleza ahadi zake chini ya Mkataba wa Maelewano wa Islamabad kutasaidia kurejesha hali ya kawaida katika eneo hilo.
-
Araghchi Ahoji Jordan: Iran Isubiri Muda Gani Kabla ya Kujibu Uchokozi?
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amepinga madai ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan kwamba shambulio la Iran dhidi ya nchi za eneo lilikuwa si majibu kwa sababu lilitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa mashambulizi ya Marekani, akisisitiza kuwa mashambulizi hayo yalitumia anga, ardhi na maji ya nchi za Kiarabu.
-
Iran Yafanya Mazungumzo ya Simu na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia na Uturuki
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amezungumza kwa simu na mawaziri wenzake wa Saudi Arabia na Uturuki kuhusu masuala ya pande mbili, maendeleo ya kikanda na juhudi za kidiplomasia za kurejesha utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Waziri Mkuu wa India: Pakistan Ikifanya Uvunjifu wa Amani, Tutaingia Katika Ardhi Yake Dondoo
Narendra Modi ameonya kuwa India iko tayari kuingia katika ardhi ya Pakistan endapo nchi hiyo itafanya vitendo vya kigaidi ndani ya India.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ampokea Balozi Mdogo Mpya wa Iran Jijini Basra
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amekutana na Mustafa Tarfi, Konseli Mkuu mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jijini Basra, Iraq, na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo, hususan katika nyanja za kiuchumi na huduma za kibalozi.
-
Waziri Mhe.Deus Sangu Akutana na Waislamu na Viongozi wa Kiislamu katika Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Kigogo Post, Dar -es- Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu, ameshiriki katika hafla ya kumbukizi ya mazazi ya Mtume Muhammad (saww), iliyowakutanisha viongozi mbalimbali wa dini na serikali katika uwanja wa Kigogo Posti, Jijini Dar es Salaam.
-
Balozi wa Iran atoa wito wa kulaaniwa kwa ugaidi wa kiuchumi wa Marekani
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uingereza, Ali Matinfar, ametoa wito wa kulaaniwa kwa mashambulizi ya kijeshi ya Marekani, uhalifu wa kivita na kile alichokitaja kuwa ni ugaidi wa kiuchumi unaofanywa dhidi ya Iran.
-
Qalibaf: “Scott, uaminifu wako uko hatarini; himaya ya Marekani inaelekea kutoweka”
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amemjibu Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, akisema uaminifu wake uko hatarini na kwamba himaya ya Marekani inaelekea kutoweka.
-
Iran yabadilisha mizani ya nguvu katika eneo, asema Waziri wa Ulinzi
Waziri wa Ulinzi na Usaidizi wa Vikosi vya Jeshi wa Iran, Brigedia Jenerali Majid Ibn al-Ridha, amesema Iran imeweza kubadilisha kwa vitendo mizani ya nguvu katika eneo na kuthibitisha kuwa enzi ya sera ya “piga na kukimbia” imekwisha.
-
Iran: Njia ya muda ya kupitisha meli katika Mlango wa Hormuz imekubaliwa na Oman
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema Iran na Oman zimekubaliana kuhusu njia ya muda ya kupitisha meli katika Mlango wa Hormuz, yenye upana wa maili 7. Amesema ufunguaji kamili wa mlango huo utategemea masharti na mipangilio itakayowekwa na Iran, huku akisisitiza kuwa Tehran bado iko katika hali ya vita.
-
Araghchi: Kujitolea kwa Iran kwa amani na utulivu kunaambatana na diplomasia endelevu na nchi jirani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema dhamira ya Iran ya kudumisha amani na utulivu inaenda sambamba na diplomasia thabiti na endelevu na nchi jirani, akisisitiza umuhimu wa kutafuta suluhisho za kikanda kwa changamoto zinazolikabili eneo.
-
Iran na Pakistan zakubaliana kuendeleza mashauriano kwa ajili ya amani na usalama wa kikanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, na Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Field Marshal Asim Munir, wamefanya mazungumzo ya simu na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza mashauriano na juhudi za pamoja kwa ajili ya kuimarisha amani na usalama katika eneo.
-
Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Waondoka Tehran
Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan wameondoka Tehran Jumatatu jioni, baada ya kumaliza ziara yao ya siku moja. Mazungumzo yao yalihusu kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na Iran, pamoja na maendeleo ya kikanda na umuhimu wa kushirikiana katika kukuza amani, utulivu na usalama wa eneo.
-
Iran: Vita la hivi karibuni yaweka upya vipaumbele na mwelekeo wa viwanda vya ulinzi
Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema vita la hivi karibuni limeibua hitaji la kuainisha upya vipaumbele vya sekta ya ulinzi, huku uzalishaji wa baadhi ya vifaa vya kijeshi ukiongezeka hadi mara kadhaa licha ya vita.
-
Iran: Baadhi ya Mabomu Yalikuwa Yametengenezwa Maalum kwa Ajili ya Kuishambulia Iran
Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Ibn al-Ridha, amesema adui alitumia mchanganyiko wa zana za kijeshi, mtandao, vikosi vya vibaraka na wapinzani wa ndani katika vita dhidi ya Iran, huku baadhi ya silaha zikitumiwa kwa mara ya kwanza na baadhi ya mabomu yakitengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuishambulia Iran.
-
Khatibzadeh: Wananchi wa Iran pia watashinda dhidi ya ugaidi wa kiuchumi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, amesema serikali ya Iran imedhamiria kukabiliana na vikwazo vya Marekani na kupunguza athari zake, huku akisisitiza kuwa wananchi wa Iran wana uwezo wa kushinda changamoto za kile alichokiita ugaidi wa kiuchumi.
-
Khatibzadeh: Mhimili wa kigaidi umeshindwa, Iran iko tayari kuwawajibisha magaidi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, amesema kile alichokiita “mhimili wa kigaidi” kimeshindwa kufikia malengo yake dhidi ya Iran, akisisitiza kuwa Tehran imeazimia kuwawajibisha wahusika wa vitendo vya kigaidi dhidi ya nchi hiyo.
-
Gharibabadi: Dhana potofu ya Trump kuhusu Mlango wa Hormuz itasahihishwa hivi karibuni
Iran: Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya Kisheria na Kimataifa, Kazem Gharibabadi, amejibu hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuchapisha ramani inayoonyesha Mlango wa Hormuz kama “ardhi mpya ya Marekani”, akisema kuwa “dhana potofu ya Trump kuhusu Mlango wa Hormuz itasahihishwa hivi karibuni.”
-
Abbas Araghchi kuzungumzia utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwa miaka miwili iliyopita
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anatarajiwa kuzungumza kupitia televisheni ya Iran kuhusu utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
-
Waziri Mkuu wa Malaysia: Kusimama imara kwa Iran dhidi ya uchokozi kunastahili pongezi
Waziri Mkuu wa Malaysia amelaani uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, akisema kuwa msimamo, azma na uvumilivu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashambulizi hayo unastahili pongezi.
-
Araghchi kwa Marekani: Mmefanya kosa kubwa sana kuhusu Mlango wa Hormuz
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema udhaifu wa kijasusi wa Marekani na tathmini zake potofu umeisababisha kufanya makosa makubwa, akisema vita dhidi ya Iran ni mfano wa wazi wa makosa hayo.