Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Muhammad Shi'ai Al-Sudani , Waziri Mkuu wa Iraq katika hotuba yake kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Imam Ali (AS) amesema: Karne kumi na nne (14) zilizopita, katika siku kama hii ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ulimwengu ulishuhudia tukio kubwa na maafa makubwa.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Ofisi ya Habari ya Waziri Mkuu wa Iraq, al-Sudani alisema: Imam Ali (a.s.) alifariki dunia kimwili, lakini uwepo wake unaendelea kwa sababu aliacha nyuma yake urithi ambapo tabia na maadili yote ya juu ya Binadamu yanadhihirika (ndani ya urithi huo).
Aliongeza: "فُزْتُ وَ رَبِّ الْکَعْبَة" / "Ninaapa kwa Jina la Mola wa al-Kaaba kwamba hakika nimefuzu" huu sio usemi wa kimhemko, lakini ni mtazamo wa (kiakhlaq) kimaadili unaotegemea wazo kamili la mageuzi ya Mwanadamu, mkabala na kifo na chaguzi za maisha.
Waziri Mkuu wa Iraq aliendelea kusema: Mageuzi ya kidunia ya Imamu huyu (amani iwe juu yake) hayajitenganishi na hadhi yake ya maisha ya baada ya kifo, ambayo hutupelekea sisi kufaidika na kuwepo kwake kwa maneno (kauli) na vitendo.
Al-Sudani amesema: Katika vita ambavyo Imam Ali (a.s) alilazimishwa kufanya (kuvipigana), Ubinadamu wake ulikuwa mbele ya upanga wake.
Akaongeza: Ubinadamu (utu) mkubwa wa Imam Ali (a.s) ulifikia kilele chake pale alipotoa nasaha kuhusu wafungwa (siku zote alikuwa akisisitiza mno juu ya suala la kujali haki za wafungwa na kutowatendea dhulma), na kutoa udhuru kwa makosa ya watu ili wapate fahamu zao.
Waziri Mkuu wa Iraq aliendelea kusema: Maisha ya Imam Ali (a.s) katika utawala wake yalikuwa ni alama ya maana zote za wema na kujali (na kuthamini) watu.
Al-Sudani akabainisha: Katika utawala wa Imam huyu (amani iwe juu yake), watu wote walikuwa sawa na hakuna aliyekuwa na kipaumbele juu ya wengine isipokuwa kwa daraja la wema, usafi wa mikono na usafi wa nafsi. Kwa msingi huu, Imam Ali (a.s) aliandika Katiba kwa ajili ya Umma na Watawala.
Ameongeza kuwa: Imam Ali (a.s) aliandika (agano) mapatano ya kina ya kiutawala kwa ajili ya Malik al-Ashtar, ambaye alikuwa Gavana wake nchini Misri, ndani yake yakiwemo maelekezo juu ya kupambana na ufisadi, kutoa wito wa kuendelezwa ardhi, kwa kutumia rasilimali zake, kuwatunza (kuwajali) masikini na kupiga vita sababu za Umasikini.
Waziri Mkuu wa Iraq ameashiria: Roho na maisha ya Amirul-Mu’minin (a.s) yanapaswa kuunganisha mwili wa Umma wa Kiislamu kama kiungo kimoja, Umma ambao leo hii unahitajia zaidi umoja huu kuliko wakati mwingine wowote, hasa katika hali ambayo maadui wake wameongezeka.
Mwishoni, mwa hotuba yake, Al-Sudani alisisitiza: Gaza inateseka, Lebanon imejeruhiwa na mikoa mingine, migogoro yote hii inatulazimisha kuungana kwa umoja wetu, na kuwa mkono usiokwaruzwa (usioumizwa wala kujeruhiwa) na maafa.
Your Comment