habari
-
Iran na Pakistan zakubaliana kuendeleza mashauriano kwa ajili ya amani na usalama wa kikanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, na Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Field Marshal Asim Munir, wamefanya mazungumzo ya simu na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza mashauriano na juhudi za pamoja kwa ajili ya kuimarisha amani na usalama katika eneo.
-
Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Waondoka Tehran
Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan wameondoka Tehran Jumatatu jioni, baada ya kumaliza ziara yao ya siku moja. Mazungumzo yao yalihusu kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na Iran, pamoja na maendeleo ya kikanda na umuhimu wa kushirikiana katika kukuza amani, utulivu na usalama wa eneo.
-
Hali ya kusikitisha ya mwandishi wa habari Mpalestina baada ya miaka miwili katika jela za Israel
Shirika la Wafungwa wa Palestina limechapisha picha ya mwandishi wa habari Mpalestina, Muhammad Arab, likisema kuwa mabadiliko makubwa katika sura yake baada ya miaka miwili ya kuwekwa kizuizini yanaakisi hali ya maelfu ya wafungwa wa Palestina na yanaashiria kuendelea kwa mateso na unyanyasaji dhidi yao.
-
Qalibaf: Waandishi wa Habari Ni Wapiganaji Wenye Maarifa Kama Ngome na Ukweli Kama Silaha
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema kuwa hatima ya mataifa haiamuliwi tu katika uwanja wa vita, bali pia katika uwanja wa simulizi, akisisitiza kuwa waandishi wa habari wana jukumu la kulinda ukweli, usalama wa kisaikolojia, utambulisho wa kitaifa na nguvu ya kiutamaduni ya taifa.
-
Wanahabari ni Wasimuliaji wa Ukweli na Mashahidi wa Zama
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRNA), Hussein Jaberi Ansari, ametembelea mji wa Borujerd katika maadhimisho ya Siku ya Wanahabari nchini Iran, akisisitiza umuhimu wa wanahabari kama wasimuliaji wa ukweli na mashahidi wa matukio ya zama zao.
-
Chanzo cha Kijeshi cha Iran:
Iran Itajibu Shambulio Lolote la Marekani Dhidi ya Miundombinu Yake kwa Kulenga Miundombinu ya Kimkakati Yenye Maslahi ya Marekani Katika Eneo
Chanzo cha kijeshi cha Iran kimesema kuwa iwapo Marekani italenga daraja au kituo chochote cha umeme nchini Iran, Iran itajibu kwa kulenga miundombinu na madaraja katika eneo hilo, ikiwemo vituo vya nishati ambavyo Marekani ina maslahi ndani yake. Chanzo hicho kimesema pia kuwa Marekani ilipaswa kutambua katika siku 10 zilizopita kwamba Iran ina uwezo wa kulenga eneo lolote itakaloamua kulishambulia.
-
Meya wa Tehran: Trump hatakuwa salama popote duniani baada ya mauaji ya Kiongozi wa Iran
Meya wa Tehran, Alireza Zakani, amesema kuwa wale wanaohusika na kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, watakabiliwa na hatua za kulipiza kisasi, akisema kuwa Rais wa Marekani Donald Trump "hatakuwa salama popote duniani."
-
Iran na Urusi Zakubaliana Kuimarisha Ushirikiano wa Haki za Binadamu na Kukabiliana na Simulizi la Magharibi
Iran na Urusi zimekubaliana kuinua kiwango cha mazungumzo yao kuhusu haki za binadamu na kuandaa mtazamo mpya wa pamoja wa kukabiliana na simulizi wanazoliona kuwa la upande mmoja kutoka mataifa ya Magharibi.
-
Iran Yatangaza Mpango Kabambe wa Anga za Juu wa 2026, Yazindua Mradi wa Satelaiti 24 za “Shahid Soleimani”
Shirika la Anga za Juu la Iran limetangaza mipango mikubwa ya mwaka 2026, ikiwemo kuzindua satelaiti ya kwanza ya rada iliyotengenezwa nchini, kuendeleza mradi wa satelaiti 24 za “Shahid Soleimani” na kuharakisha maendeleo ya satelaiti za mawasiliano na uchunguzi wa ardhini.
-
Iran yaokoa mabaharia 23 baada ya meli mbili kugongana katika Ghuba ya Uajemi
Mamlaka ya Bandari na Usafiri wa Baharini ya mkoa wa Hormozgan nchini Iran imefanikiwa kuwaokoa mabaharia 23 baada ya meli mbili za mizigo kugongana katika maji ya pwani ya Bandar Abbas.
-
Mwanasiasa wa Pakistan: Kiongozi Shahidi Imam Khamenei Aliifanya Iran Kuwa Taifa la Mapambano na Kuunganisha Umma Dhidi ya Uzayuni
Naibu Kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan, Liaqat Baloch, amesema Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (r.a.) aliiongoza Iran kwa misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuifanya kuwa taifa la mapambano, huku akisisitiza umoja wa Umma wa Kiislamu na uungaji mkono wa kudumu kwa Palestina.
-
Mzunguko wa Kwanza wa Mazungumzo ya Uswisi Wafikia Makubaliano Matano Muhimu Kuhusu Iran
Kamati ya habari ya timu ya mazungumzo ya "Minab 168" imetangaza kuwa mzunguko wa kwanza wa mazungumzo yaliyofanyika mjini Bürgenstock, Uswisi, umefikia makubaliano matano muhimu yanayohusu usalama wa Lebanon, Mlango wa Hormuz, mpango wa nyuklia wa Iran, mali zilizogandishwa na kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vya mafuta.
-
IRGC Yakanusha Taarifa za Kuuawa kwa Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qassem
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limezitaja kuwa za uongo taarifa zinazodai kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sheikh Naim Qassem, ameuawa katika shambulio la Israel kusini mwa Beirut, likisema ni sehemu ya vita vya kisaikolojia na upotoshaji wa habari.
-
Iran Yaikosoa Rasimu ya Azimio la Marekani katika Baraza la Magavana wa IAEA, Yataja Kuwa ya Kisiasa na ya Uchochezi
Iran imeeleza kuwa rasimu ya azimio iliyowasilishwa na Marekani pamoja na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani katika Baraza la Magavana la Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ni ya kisiasa na ya uchochezi, ikidai kuwa inalenga kuhamisha lawama kutoka kwa washambuliaji kwenda kwa mhanga.
-
Somalia Yasisitiza Umoja wa Kitaifa na kwamba Ukamilifu wa Ardhi na Mamlaka ya Taifa Lake Haviwezi Kugawanyika
Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa ukamilifu wa ardhi na mamlaka ya taifa la Somalia hauwezi kugawanywa, akieleza vipaumbele vya urais wa Somalia wa Baraza la Usalama Januari 2026 na kukataa vikali hatua zozote zinazolenga kudhoofisha umoja wa nchi hiyo.
-
Zelensky: Ukraine Inatarajia Jibu la Moscow Kuhusu Rasimu ya Kumaliza Vita, Ikiikataa Sharti la NATO
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ameiweka wazi kuwa anatarajia kupokea jibu la Moscow leo Jumatano kuhusu rasimu mpya ya pendekezo la kumaliza vita, iliyokubaliwa awali kati ya Washington na Kyiv. Hata hivyo, Zelensky amesisitiza kuwa Ukraine haitaweza kukubali sharti lolote linalohusiana na kujiunga au kutokuwa mwanachama wa NATO, jambo ambalo Urusi ilikuwa imependekeza, akionyesha wazi kuwa suala hilo haliwezi kuwa kikwazo cha mazungumzo ya amani.
-
Mwandishi wa habari wa Marekani aliyekuwa mkosoaji wa serikali ya Julani akamatwa na kupelekwa kusikojulikana
Tangu kuingia madarakani, serikali ya Ahmed al-Shar‘a, anayejitambulisha kama rais wa Syria, imekuwa ikizidi kubana uhuru wa maoni na kujieleza, na imewakamata watu kadhaa, wakiwemo baadhi ya walio na ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii.
-
Habari Kuhusu Makubaliano ya “Mfumo wa Uratibu wa Vyama vya Kishia Iraq” Juu ya Mgombea wa Uwaziri Mkuu
Vyanzo vya kisiasa vya Iraq vimeripoti kuwepo kwa makubaliano ya awali miongoni mwa vyama vinavyounda muungano wa “Mfumo wa Uratibu wa Vyama vya Kishia Iraq” kuhusu uteuzi wa mgombea wa kuongoza serikali ijayo ya nchi hiyo.
-
Jeshi la Lebanon liliwaruhusu waandishi wa habari kuingia katika vituo vya Hizbullah;
JKituo cha kihistoria cha Muqawama ambacho ukweli wake umejulikana baada ya kusitishwa kwa mapigano
Bonde la Zabqin, kutokana na muundo wake maalum wa kijiografia na umbali wa takribani kilomita 10 kutoka mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, linachukuliwa kuwa mojawapo ya ngome kuu za Muqawama (Upinzani). Ni ngome ambayo vizazi mbalimbali vya wapiganaji wa Kipalestina na Wenyeji wa Lebanon wamekuwa wakikuwapo humo kwa miaka mingi.
-
Nafasi Muhimu ya Nahjul-Balagha katika Elimu ya Bara Hindi:
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as) na Kituo cha Fikra za Kiislamu Waandaa Webina ya Kimataifa Kuhusu Nafasi Muhimu ya Nahjul-Balagha katika Elimu
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kwa kushirikiana na Kituo cha Fikra za Kiislamu wameandaa webina ya kimataifa iliyopewa jina: “Hadhi ya Nahj al-Balagha katika Bara la Hindi na Nafasi Yake katika Elimu.” Tukio hili limefanyika Jumamosi, tarehe 15 Novemba 2025.
-
Usalama wa kisaikolojia katika familia ya Kiislamu؛ mstari wa mbele wa vita vya kifikra
Katika wakati ambapo shambulio za kifikra zinachukua lengo la amani ya nyumbani, familia ya Kiislamu, kwa kuunganishwa kwa imani, upendo na mazungumzo, huunda ngome ya kwanza ya usalama wa kisaikolojia; ni mahali ambapo amani ya kiungu inasimama dhidi ya hofu zinazotokana na vyombo vya habari, na kiroho hubaki kuwa kimbilio la faraja na uhakika wa mioyo.
-
Katika Kikao cha "Nafasi ya Wanawake wa Vyombo vya Habari katika Muqawama (Mapambano - Upinzani) ilibainika:
Kutoka kwa Zainab al-Kubra(s) hadi leo; Karbala ni Chuo cha Habari cha Mwanamke Muumini /Wanawake Waislamu wako mstari wa mbele katika vita vya Habari
Misingi Mitatu ya Wajibu wa Mwanamke Mwislamu katika Ulimwengu wa Habari Kueneza uelewa: Mwanamke Mwislamu anapaswa kuwa sauti ya ukweli, afichue upotoshaji wa vyombo vya habari vya upande wa uongo, na atangaze mateso ya waliodhulumiwa duniani – kuanzia Palestina hadi kila sehemu inayokandamiza utu. Kutetea utambulisho: Vyombo vya habari vya kisasa vinajaribu kumvua mwanamke heshima yake na kumgeuza bidhaa ya matangazo. Mwanamke Mwislamu lazima athibitishe kuwa uhalisia na usasa vinaweza kuishi pamoja, na kwamba heshima hupimwa kwa utiifu wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu, si kwa uchi au mvuto wa sura. Kulea kizazi cha waandishi wa kweli: Wajibu wa mwanamke hauishii katika kushiriki binafsi katika vyombo vya habari; anatakiwa kulea kizazi kinachotambua nguvu ya neno na dhamana ya uandishi wa ukweli.
-
Hasira za Wazayuni kutokana na kushindwa kwao Gaza / Hamas na Muqawama bado wapo imara
Shirika la televisheni la Kizayuni Channel 12 limekiri kwamba: “Hamas, katika kipindi cha miaka miwili migumu sana ikiwemo vita ya hivi karibuni, imeonyesha ujasiri na haijashindwa. Lengo kuu la Israel katika vita - yaani ‘kuishinda Hamas’ - halijafanikiwa.”