Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- baada ya kupita miaka miwili tangu kuanza kwa operesheni “Tofaan al-Aqsa (Dhoruba ya Al-Aqsa)”, makubaliano ya kusitisha mapigano kwa awamu ya kwanza kati ya Hamas na Israel yamefanikishwa kwa upatanishi wa Qatar na Misri.
Baada ya makubaliano hayo ya kusitisha vita kati ya utawala wa Kizayuni na Hamas, sasa viongozi na vyombo vya habari vya Kizayuni wameanza kukosoa sera za Waziri Mkuu na baraza lake la vita, wakizungumza kuhusu mwisho mchungu wa miaka miwili ya mapigano yasiyo na matokeo Gaza, huku Hamas ikibaki imara na ikionekana mshindi.
Gazeti la Kizayuni Haaretz limeandika kuwa:
“Vita vya Gaza vinakaribia kufikia mwisho wake, lakini hilo si ishara ya ushindi wa kweli kwa Israel. Hamas imetoka salama katika mapigano haya, imefanikiwa kuwaachia huru wafungwa wa Kipalestina, na suala la Palestina limewarejelea tena kwenye uwanja wa kimataifa, ilhali Tel Aviv haijapata ushindi wowote wa kweli katika Ukanda wa Gaza.”
Yoni Ben Menachem, mtafiti wa Kizayuni kutoka Kituo cha JCFA, katika Channel 14 ya Israel alisema:
“Hakuna uwezekano wowote kwamba Hamas itaweka silaha zake chini. Israel bila msaada wa Trump haina ruhusa ya kufanya chochote hata kidogo.”
Mmoja wa wabunge wa Knesset naye alikiri kutengwa kwa Israel duniani, akimwambia Waziri Mkuu wa utawala huo:
“Bwana Netanyahu, umethibitisha kwamba tumeachwa peke yetu duniani. Hotuba yako katika Umoja wa Mataifa ilitolewa ndani ya ukumbi ulio tupu; watu waliondoka, na waliobaki waliokushangilia walikuwa ni wajumbe wa Israel na Marekani pekee.”
Meir Javedanfar, mtaalamu wa masuala ya Kizayuni anayezungumza Kifarsi, naye alikiri kwamba:
“Hamas haitaharibiwa; Israel imelazimika kukubali kusitisha mapigano kwa kutoa masharti na ustahimilivu wa maumivu makubwa.”
Mwishoni, Channel 12 ya televisheni ya Kizayuni ilikiri tena kuwa:
“Hamas, katika kipindi cha miaka miwili migumu sana ikiwemo vita ya hivi karibuni, imeonyesha ujasiri na haijashindwa. Lengo kuu la Israel katika vita, yaani ‘kuishinda Hamas,’ halijatekelezwa.”
Your Comment