Operesheni
-
Burkina Faso, Mali na Niger Zazindua Operesheni ya Pamoja ya Kijeshi Dhidi ya Makundi ya Kijihadi
Kiongozi wa mpito wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré, ametangaza kuanza kwa hatua mpya za kijeshi katika eneo la Sahel baada ya nchi yake, kwa kushirikiana na Mali na Niger, kuzindua operesheni ya pamoja inayolenga kukabiliana na makundi ya kijihadi yanayohusishwa na Al-Qaeda na ISIS. Hatua hiyo inakuja katika muktadha wa kuimarishwa kwa muungano wa kijeshi wa nchi hizo tatu, huku zikisisitiza mshikamano wa kiusalama na mwelekeo mpya wa ushirikiano wa kikanda kufuatia kujiondoa kwao katika ECOWAS na kuvunja ushirikiano wa awali na Ufaransa na Marekani.
-
Habari za Hivi Punde | Iran Yakamata Meli Iliyokuwa Inasafirisha Lita Milioni 4 za Mafuta ya Magendo katika Ghuba ya Uajemi
Maafisa wa Iran wamesisitiza kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi endelevu za kupambana na magendo ya rasilimali za taifa, kulinda uchumi wa nchi, na kudumisha usalama wa majini katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Putin Aahidi Urusi Kuchukua Eneo la Donbas kwa Njia Zote, Wakati Waukrainia Wakiandaa Mazungumzo Za Amani na Marekani
Putin alifika New Delhi, India, Alhamisi, ambapo alikaribishwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, siku mbili tu baada ya mkutano wake katika eneo la Kremlin na ujumbe wa Marekani ulioongozwa na mwakilishi maalum Steve Witkoff.
-
Trump: Hivi karibuni tutaanzisha operesheni ya kijeshi ya ardhini nchini Venezuela
Rais wa Marekani ametangaza kuongezwa kwa mashambulizi kutoka baharini hadi ndani ya ardhi ya Venezuela, na kusema kuwa Washington “hivi karibuni sana” italenga njia za ardhini zinazotumiwa kwa magendo.
-
Utawala wa Kizayuni: “Kabla ya kushambulia Iran, lazima kwanza kudhoofisha Hizbullah / Kaskazini lazima itulie ndipo iwezekane kuivamia Iran!”
Utawala wa Israel umekaza vitisho vyake kuhusu kuanzisha awamu mpya ya mapigano ya kijeshi dhidi ya Lebanon. Lengo lililotangazwa la operesheni hii ni kuzuia kujengwa upya kwa uwezo wa kijeshi wa Hizbullah na kulazimisha serikali ya Lebanon kutekeleza mpango wa kulivua silaha kundi hilo.
-
Kiongozi wa Harakati ya Hamas: Ghaza imejeruhiwa lakini imebaki yenye nguvu; Ummah wa Kiarabu unapaswa kuimarisha uwezo wake wa upinzani
Kiongozi wa Harakati ya Hamas, katika Ukanda wa Ghaza, katika Kongresi ya 34 ya Taifa ya Kiarabu huko Beirut, alieleza kuwa Operesheni “Tofaan Al-Aqsa / Kimbunga cha Al-Aqsa” ilikuwa jibu kwa juhudi za kuondoa suala la Palestina na kubuni Mashariki ya Kati mpya, na alisisitiza uhitaji wa kuimarisha uwezo wa upinzani.
-
Hamdan Sabbahi: Operesheni “Tofaan Al-Aqsa” imevunja njia ya kawaida ya uhusiano na Israeli
Hamdan Sabbahi, katika hotuba yake Beirut, akionyesha athari za Operesheni “Kimbunga cha Al-Aqsa”, alisisitiza juu ya kushindwa kwa miradi ya kutaka kugawanya ardhi na kukawaidaisha uhusiano na utawala wa Kizayuni, na pia alibainisha kuwa utetezi wa silaha za upinzani na nafasi ya vyombo vya habari itakuwa muhimu sana katika vita vya siku zijazo.
-
Hasira za Wazayuni kutokana na kushindwa kwao Gaza / Hamas na Muqawama bado wapo imara
Shirika la televisheni la Kizayuni Channel 12 limekiri kwamba: “Hamas, katika kipindi cha miaka miwili migumu sana ikiwemo vita ya hivi karibuni, imeonyesha ujasiri na haijashindwa. Lengo kuu la Israel katika vita - yaani ‘kuishinda Hamas’ - halijafanikiwa.”
-
Magaidi 10, Wakiwemo Wanawake Wawili, Watekwa na Shirika la Taarifa za Kijajusi la Kijeshi la Iraq
Shirika la Taarifa za Kijeshi la Iraq leo limetangaza kuwa katika operesheni mbalimbali za kiusalama, limefanikiwa kuchukua watu 10 wa kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi, wakiwemo wanawake 2.
-
"Tufani ya Al-Aqsa”: Jibu kwa Swali na kwa Miaka ya Uvunjaji wa Haki na Ukaliaji kwa Mabavu"
Swali la kihistoria tunalotakiwa kulitolea Majibu ya Kihistoria na ya ndani ya nafsi zetu ni hili: Katika mapambano kati ya jeshi la Mwenyezi Mungu na jeshi la Shetani, sisi tunatakuwa kusimama upande upi?.
-
Kuimarishwa kwa hatua za kiusalama katika mji mkuu wa Iraq kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu
Kamanda wa operesheni za Baghdad ametangaza kuanza kwa mpango mpya wa kukabiliana na wizi wa magari na mauaji katika mji mkuu wa Iraq.
-
Kuanza kwa Operesheni ya Kijeshi Katika Bonde la Al-Shay, Kirkuk kwa Lengo la Kuangamiza Maficho ya ISIS
Vyanzo vya usalama vya Iraq vimetangaza kuwa operesheni maalum ya kijeshi imeanza katika sehemu ya mashariki ya Bonde la Al-Shay, karibu na mji wa Kirkuk.
-
Ufichuzi wa uvamizi mkubwa zaidi wa Jeshi la Israel ndani ya ardhi ya Syria tangu kuanguka kwa Serikali ya Bashar al-Assad
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Israel wamedhibiti ukanda wa kilomita 10 kuanzia eneo la Golan hadi Hamat Ghadeer, na kuanzisha kambi mpya 8 za kijeshi katika eneo hilo.
-
Mwandishi maarufu wa Iraq afichua:
Operesheni za kuzunguka (mbinu za ujanja) kwa mtindo wa Kimarekani; Vita vinavyoitwa amani
"Abbas al-Zaydi", Mwanaharakati wa vyombo vya habari kutoka Iraq, ameandika katika makala yake kwamba: Marekani, kwa jina la amani, inaendeleza vita vyake vya hivi karibuni dhidi ya dunia kwa njia kadhaa, ambazo huenda muhimu zaidi kati ya hizo ni kupitia miungano kama NATO, utawala wa Kizayuni wa Israel, na magenge ya kigaidi.
-
“Msikiti; Kitovu cha Umoja na Ngome ya Mapambano” Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Msikiti
Tehran – Katibu wa Kituo cha Kitaifa cha Msikiti, Hujjatul-Islam Ali Nouri, ametangaza kuwa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Msikiti mwaka huu yatafanyika kuanzia tarehe 31 Mordad hadi 7 Shahrivar (sawa na 22–29 Agosti 2025) katika ngazi ya kitaifa, mikoa na wilaya, chini ya kaulimbiu: “Msikiti, Kitovu cha Umoja, Ngome ya Mapambano.”
-
Kuanza kwa Mchakato wa Kuondoka Kikamilifu kwa Vikosi vya Marekani kutoka Baghdad kuelekea Erbil Mwezi Septemba
Chanzo cha serikali ya Iraq kimetangaza kuwa vikosi vya Marekani vitaanza mchakato wa kuondoka kikamilifu mjini Baghdad kuanzia mwezi Septemba 2025 na kuhamia Erbil, mji mkuu wa eneo la Kurdistan nchini Iraq.
-
Jeshi la Iran:
"Majibu ya Iran yatakuwa makali zaidi iwapo adui atafanya kosa”
Jeshi Kuu la Iran lilibainisha kuwa katika tukio la kosa la kimahesabu kutoka kwa adui, kile kilichozuia operesheni kubwa wakati wa vita vya siku 12 vilivyopita hakitarudiwa tena.
-
Shehena ya Mirungi kutoka Kenya Yanaswa Baharini na Polisi Tanga Katika Msako Maalum
Jeshi linasisitiza ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya dola katika kukomesha biashara na usafirishaji wa dawa za kulevya nchini.
-
Wananchi wa Yemen wanalenga (wanashambulia) maeneo mbalimbali ya Wazayuni kujibu jinai zinazoendelea kufanywa na Israel
Vikosi vya jeshi la Yemen vimeanzisha operesheni mpya ya ndege zisizo na rubani dhidi ya utawala wa Israel, hatua ambayo kwa mujibu wa duru za Yemen, ilifanyika kujibu mauaji ya raia huko Gaza.
-
Khartoum imeachiliwa huru; jeshi la Sudan limetangaza kuwa limekamilisha operesheni ya usafishaji (kuondoa vikosi vya adui)
Jeshi la Sudan limetangaza kuwa limekamilisha usafishaji wa Khartoum kutoka kwa Vikosi vya Radiamali ya Haraka na limeushutumu Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kuingilia kati kijeshi katika mzozo huu.
-
Hakim: Hashd al-Shaabi ina Jukumu la msingi katika kuilinda Iraq
Kiongozi wa Harakati ya Hekima ya Kitaifa ya Iraq amesisitiza umuhimu wa Hashd al-Shaabi katika kulinda nchi ya Iraq na ametoa wito wa kuendelezwa kwa juhudi za kiusalama pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika uwanja huo. Sayyid Ammar Hakim pia ameashiria kujitolea kwa Hashd al-Shaabi na nafasi yake katika kuleta uthabiti nchini Iraq, na amesisitiza ulazima wa kulinda heshima na sifa njema ya taasisi hiyo.