14 Septemba 2025 - 12:06
Ufichuzi wa uvamizi mkubwa zaidi wa Jeshi la Israel ndani ya ardhi ya Syria tangu kuanguka kwa Serikali ya Bashar al-Assad

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Israel wamedhibiti ukanda wa kilomita 10 kuanzia eneo la Golan hadi Hamat Ghadeer, na kuanzisha kambi mpya 8 za kijeshi katika eneo hilo.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Gazeti la Yedioth Ahronoth limeripoti kuwa Jeshi la Israel limepenya kilomita 38 ndani ya ardhi ya Syria; operesheni ambayo imeelezwa kuwa ni hatua kubwa zaidi ya kijeshi tangu kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad.

Katika operesheni hiyo iliyopewa jina la “Kijani na Nyeupe”, Jeshi la Israel limefanikiwa kuteka kambi mbili za kijeshi za Syria bila mapigano, na kuchukua zaidi ya tani 3.5 za silaha na risasi, zikiwemo makombora, mizinga ya mabomu na tanki.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Israel wamedhibiti ukanda wa kilomita 10 kuanzia eneo la Golan hadi Hamat Ghadeer, na kuanzisha kambi mpya 8 za kijeshi katika eneo hilo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha