uvamizi
-
Sheikh Naeem Qassem: Sisi ni watoto wa Imam Hussein (a.s) na hatuoni chaguo isipokuwa kuishi kwa heshima
Katibu Mkuu wa Hizbullah alipozungumza kwa ajili ya Siku ya Shahidi alisema: hatutaachana na silaha inayoitwawezesha kujitetea. Tumeachwa kwa shambulio na tutajilinda wenyewe.
-
Lebanon Yakatishwa Tamaa na Msaada wa Kimataifa Dhidi ya Uvamizi wa Israel / Shinikizo Linaloongezeka la Kuilazimisha Hizbullah Kuweka Silaha Chini
Aoun: “Tumeziomba nchi rafiki za Lebanon zisaidie kuishinikiza Israel kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano, lakini hadi sasa hakuna matokeo chanya yaliyopatikana.”
-
Shariatmadar katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya “Wakili”:
Sayyid Isa Tabatabaei alitia roho ya mapambano ndani ya jamii ya Kishia / Mradi bado kuna uvamizi, basi mapambano yataendelea kuishi
Kaimu balozi wa zamani wa Ofisi ya Utamaduni wa Iran nchini Lebanon na mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) amesema: “Iwapo Imam Musa Sadr ndiye aliyeweka misingi ya taasisi za kijamii na kitamaduni za Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, basi Sayyid Isa Tabatabaei ndiye aliyepulizia roho ya mapambano ndani ya jamii hiyo na kuifanya roho ya mapambano iwe sehemu ya utambulisho wao.” Kutokana na juhudi zake, harakati ya mapambano ya kisasa nchini Lebanon ilizaliwa — mapambano yaliyofikia kilele chake katika kuunga mkono dhana ya Palestina.
-
Waziri wa Ulinzi wa Yemen: Tuko tayari kukabiliana na uvamizi wowote unaoweza kufanywa na adui
“Mohammed Nasser al-Atifi,” Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Sana’a, akitoa pole kwa viongozi wakuu wa nchi kufuatia kuuawa kwa Mkuu wa Majeshi, alisisitiza kuwa: Tuko tayari kikamilifu katika nyanja zote za kijeshi kukabiliana na shambulio au uvamizi wowote unaoweza kutokea.
-
Hamas: Kuweka veto kwa Azimio la Gaza kunaonesha ushirikiano wa Marekani katika uhalifu wa Israel
Harakati ya Kiislamu ya Mapambano ya Palestina, Hamas, siku ya Ijumaa ilitangaza kuwa kura ya turufu (veto) ya Marekani dhidi ya azimio kuhusu Gaza ni uthibitisho wa wazi na kamili wa ushirikiano wake katika uhalifu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina walioko Ukanda wa Gaza. Hamas imesema kuwa hatua hiyo inaonesha kuwa Marekani inasaidia moja kwa moja mashambulizi, mauaji na uharibifu unaofanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia, na siyo tena mpatanishi wa haki katika mgogoro huo. Vilevile, harakati hiyo imeitaka jumuiya ya kimataifa kusimama imara dhidi ya upendeleo huu na kuchukua hatua za dharura kuwalinda Wapalestina na kukomesha uvamizi wa Israel.
-
UNIFIL: Israel iache mara moja uvamizi dhidi ya Lebanon
UNIFIL imeitaka jeshi la Israel kusitisha mara moja mashambulizi ya anga dhidi ya Lebanon na kuondoka kabisa kutoka katika ardhi ya Lebanon.
-
Ufichuzi wa uvamizi mkubwa zaidi wa Jeshi la Israel ndani ya ardhi ya Syria tangu kuanguka kwa Serikali ya Bashar al-Assad
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Israel wamedhibiti ukanda wa kilomita 10 kuanzia eneo la Golan hadi Hamat Ghadeer, na kuanzisha kambi mpya 8 za kijeshi katika eneo hilo.
-
Taarifa ya Hizbullah na Harakati ya Amal zinatoa wito wa mkusanyiko wa kuonyesha upinzani dhidi ya maamuzi ya serikali
Katika taarifa ya Hizbullah na Harakati ya Amal ilisemwa: 'Enyi wafanyakazi na wazalishaji wa Lebanon, tumekuwa wavumilivu kwa muda mrefu juu ya changamoto zinazolikumba taifa letu, na sasa umefika wakati wa kuonyesha msimamo wetu wa kitaifa kwa pamoja.' Wakaongeza: 'Tuna miadi ya kusimama kwa pamoja kama taifa, kuonyesha kupinga kwetu njia ya kujisalimisha na kutii bila masharti, na kulinda nguvu na uhuru wa Lebanon'.
-
Uvamiaji Mkubwa wa Vikosi vya Israel katika Vijiji vya Kusini mwa Syria
Katika mwendelezo wa operesheni za kijeshi za utawala wa Israel ndani ya ardhi ya Syria, doria kadhaa za jeshi la Israel zimeingia katika vijiji vya mkoa wa Quneitra na kufanya ukaguzi wa nyumba za wananchi.
-
Uungaji mkono mkubwa wa Maraaji Taqlid kwa Ayatollah Khamenei:
Sapoti kubwa ya Marajii Taqlid wa Ulimwengu wa Kishia kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran/Jibu kali kwa manenoya udhalilishaji ya Trump
Marajii Wakuu wa Taqlid katika Ulimwengu wa Kishia, Ayatollah: Sistani, Makarem Shirazi, Nouri Hamedani, Javadi Amoli, Sobhani na Shabiri Zanjani wameshutumu katika taarifa tofauti matamshi ya udhalilishaji ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Jeshi la Israel linapanga njama ya kuteka 50% ya Ukanda wa Gaza
Jeshi la Israel linapanga kudhibiti asilimia 50 ya Ukanda wa Gaza ikiwa kutakuwa hakuna maendeleo katika mazungumzo ya pande mbili.