Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (AS) - ABNA -, Tovuti ya habari ya Kiebrania "Walla" iliripoti, ikinukuu chanzo cha usalama: Jeshi la Israel linapanga kudhibiti asilimia 50 ya Ukanda wa Gaza ikiwa hakutakuwa na maendeleo katika mazungumzo ya pande mbili.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa jeshi linakaribia kudhibiti asilimia 30 ya Ukanda wa Gaza.
Ripoti hii inakuja wakati redio ya jeshi vamizi la kizayuni iliporipoti kwamba vikosi vilivyovamia vimekamilisha ujenzi wa mhimili wa Morag, kudhibiti kabisa eneo la mhimili, na kuzunguka kabisa Brigedia ya Rafah.
Jeshi linaloikalia kwa mabavu Palestina limeongeza kuwa: Eneo la Rafah sasa limezingirwa na wanajeshi wa Israel kutoka pande zote. Vikosi vinavyoikalia palestina kimabavu vitajaribu kuiambatanisha Rafah kwenye eneo la buffer kama eneo lililo chini ya udhibiti wa vikosi vinavyokalia Palestina kimabavu.
Your Comment