Ghaza
-
Maandamano ya “Gaza” Islamabad: Hafidh Naeem atoa wito wa mgomo wa kitaifa na kususia bidhaa za Israel
“Tunaiheshimu nchi yetu, lakini tunataka kuwastua watawala ili wasimame na watu wa Palestina na Kashmir. Ummah wa Kiislamu umelala usingizi wa kutojali.”
-
Morocco; Imeshuhudia Mikusanyiko 105 ya Kuunga Mkono Palestina
Al Jazeera Qatar imeripoti kuwa, (mikusanyiko) maandamano 105 yalifanyika katika miji 58 ya Morocco katika kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Gaza.
-
Usitishaji vita wa siku 70 huko Gaza; Je, Tel Aviv itakubali na kutii makubaliano hayo?
Mazungumzo kati ya Hamas na Mamlaka ya Misri Mjini Cairo yanaendelea kufanikisha usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza. Makubaliano hayo yanajumuisha kuachiliwa kwa idadi kadhaa ya wafungwa wa Israel na Palestina na iwapo yatakubaliwa, yanaweza kusaidia kuboresha hali ya kibinadamu katika eneo hilo. Walakini, Tel Aviv bado haijajibu vyema kwa makubaliano ya mwisho.
-
Gaza katika moto, dunia katika ukimya; Wanazuoni wa Bahrain wanapiga kelele / wanapaza sauti dhidi ya jinai na ulegevu wa aibu wa nchi za Kiislamu
Huku Ghaza ikipamba moto kutokana na uvamizi wa utawala ghasibu wa Kizayuni, wanazuoni wa Bahrain kwa kauli iliyo wazi wamepongeza kusimama kidete wananchi wa Palestina na kulaani mauaji ya kudumu na kimya cha kutisha cha taasisi za kimataifa na nchi za Kiarabu.
-
Jeshi la Israel linapanga njama ya kuteka 50% ya Ukanda wa Gaza
Jeshi la Israel linapanga kudhibiti asilimia 50 ya Ukanda wa Gaza ikiwa kutakuwa hakuna maendeleo katika mazungumzo ya pande mbili.
-
Wito wa Maandamano kufuatia Mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni
Kufuatia mashambulio hayo ya kinyama ya utawala wa Kizayuni, Baraza la Uratibu wa Tabligh za Kiislamu limetoa taarifa likiwaalika Wananchi Watukufu wa Tehran kushiriki katika maandamano yatakayofanyika kesho katika Medani ya Palestina.
-
Hatua mpya katika kuhalalisha uhusiano wa kawaida; Mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Imarati (UAE ) na utawala haram wa Kizayuni
Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE Abdullah Bin Zayed amejadili uhusiano wa pande mbili katika mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kizayuni Gideon Sa'er huko Abu Dhabi. Katika kikao hicho amesisitiza juhudi za kidiplomasia za kufikia usitishaji vita huko Ghaza, lakini mkutano huu ulifanyika katika hali ambayo utawala wa Kizayuni unaendelea kuua na kufanya mauaji ya kimbari huko Ghaza.
-
Fat'wa Mpya: Kuitetea Palestina na Jihad dhidi ya Utawala wa Kizayuni ni Wajibu Ayn (jambo la faradhi kwa kila Mtu)
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Ulimwenguni umetoa Fat'wa kuhusu Wajibu wa Jihadi katika kuunga mkono Ghaza na kusisitiza kuwa, Jihadi dhidi ya utawala wa Kizayuni na mamluki na askari wake wanaohusika na mauaji ya halaiki ya watu wa Ghaza katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ni wajibu mutlaki (unaomgusa kila mtu).
-
Kuuawa Shahidi kwa Wapalestina 15 wakati wa Shambulio la bomu kwenye jengo moja huko Gaza / Hakuna mahali salama huko Gaza
Mashambulio ya kikatili ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza yameendelea hivi leo, na kwa sababu hiyo Wapalestina wengi zaidi wameuawa Shahidi.
-
Mashahidi 38 wa Kipalestina; Uovu mpya wa utawala wa Kizayuni huko Gaza
Katika muendelezo wa mashambulizi katika Ukanda wa Ghaza, utawala wa Kizayuni umeua idadi nyingine ya Wapalestina.
-
Ayatollah Nouri Hamedani: Utawala wa Kizayuni unaoua watoto kwa mara nyingine tena umeonyesha kwamba hauzingatii ahadi zozote
Ayatollah Nouri Hamedani ametoa ujumbe akilaani jinai za hivi karibuni za Marekani na utawala wa Kizayuni na kusema: Leo hii utawala wa Kizayuni unaoua watoto kwa mara nyingine umeonyesha tena kwamba haufuatilii (na hauzingatii) ahadi zozote na unavunja ahadi (mapatano) kirahisi.
-
Vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza vimeanza tena| Wapalestina 131 wameuawa Shahidi katika mashambulizi ya mabomu ya ndege za Israel
Utawala wa Kizayuni umeshambulia kwa mabomu maeneo mbalimbali ya makazi ya watu katika Ukanda wa Ghaza