Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Gaza - Kundi la Hamas limewaita karibu wapiganaji wake elfu saba (7,000) kupitia ujumbe wa njia ya simu, likiwaagiza kuimarisha uwepo wake katika maeneo yanayoachwa na wanajeshi wa Israel. Hatua hii imechukuliwa kufuatia wasiwasi wa kuibuka kwa migongano na makundi mengine yenye silaha, ikiwemo lile la jamii ya Dughmush.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, Hamas pia imewateua magavana wapya watano wenye uzoefu wa kijeshi kusimamia maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, huku baadhi ya wapiganaji wake wakiwa tayari wametumwa kutekeleza majukumu hayo.
Wachambuzi wa masuala ya usalama wanaonya kuwa hatua hiyo ya Hamas inaweza kutishia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyopo kwa sasa, ambapo pande zote zilitarajiwa kuweka chini silaha. Hata hivyo, suala la nani ataongoza Gaza baada ya makubaliano hayo linaendelea kuwa tata na lenye utata mkubwa wa kisiasa na kiusalama.
Your Comment