Washiriki katika Hafla hiyo ya Maulid Tukufu walipongeza juhudi za walimu wa Madrasa kwa kuandaa tukio lililojumuisha Elimu, Burudani ya kiroho, na Hamasa ya Kijamii, huku wakihimizwa kuendeleza umoja na ushirikiano katika Malezi ya watoto wa Kiislamu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar -es- Salaam, 11 Oktoba 2025 - Taasisi ya elimu ya Kiislamu Madrasat al_Shuhadaa iliyoko mbezi malamba mawili kwa baba mustapha leo imefanya hafla ya maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) sambamba na maonyesho maalum ya watoto wanaosoma katika madrasa hiyo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wazazi, walimu, viongozi wa dini, pamoja na wageni waalikwa mbalimbali, ambapo watoto waliwasilisha Qaswida, Mashairi, Michezo ya kuigiza ya Kiislamu, na hotuba fupi kuhusu maisha ya Mtume Mtukufu (saww).
Mwalimu Mkuu wa Madrasa hiyo, katika hotuba yake, ameeleza kuwa lengo la hafla hiyo ni kuwalea watoto katika misingi ya Mapenzi kwa Mtume (s.a.w.w), nidhamu, elimu, na maadili bora. Amesema kuwa kupitia Maulid na maonyesho kama haya, watoto hujifunza jinsi ya kuishi kwa mfano wa Mtume Muhammad (saww) katika nyanja zote za maisha.
“Tunataka watoto wetu wakue wakimjua Mtume (saww), wakimpenda, na kuiga mwenendo wake. Maulid ni sehemu ya Malezi ya Kiroho na Kijamii kwao,” alisema Mwalimu Mkuu.
Washiriki katika Hafla hiyo ya Maulid Tukufu walipongeza juhudi za walimu wa Madrasa kwa kuandaa tukio lililojumuisha Elimu, Burudani ya kiroho, na Hamasa ya Kijamii, huku wakihimizwa kuendeleza umoja na ushirikiano katika Malezi ya watoto wa Kiislamu.
Hafla imehitimishwa kwa dua maalum ya kuombea Amani, Umoja, na Mafanikio ya Taifa pamoja na kizazi kijacho cha kiislamu.
Your Comment