Sheikh Hemed Jalala: “Tuendelee kuiombea nchi yetu, viongozi wetu, na hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, ili Allah ampe Hekima, Afya, na Mafanikio katika kuongoza Taifa letu,”

12 Oktoba 2025 - 16:24

Sheikh Hemed Jalala : “Kuwatumikia Watu ni Ibada Kubwa Zaidi” - Akihutubia Hafla ya Maulid Ngarenaro - Arusha +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Arusha, 12 oktoba 2025 - Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shi'a Tanzania (T.I.C), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakingende, leo ameshiriki katika hafla tukufu ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) iliyoandaliwa na Taasisi ya Sayyid al-shuhadaa katika eneo la Ngarenaro, Mkoani Arusha.

Sheikh Hemed Jalala : “Kuwatumikia Watu ni Ibada Kubwa Zaidi” - Akihutubia Hafla ya Maulid Ngarenaro - Arusha +Picha

Hafla hiyo imejumuisha waumini, viongozi wa dini, na wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali za Arusha na Mikoa jirani, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w).

Sheikh Hemed Jalala : “Kuwatumikia Watu ni Ibada Kubwa Zaidi” - Akihutubia Hafla ya Maulid Ngarenaro - Arusha +Picha

Katika hotuba yake, Sheikh Hemed Jalala alimpongeza Sheikh Maulid Sombi, Kiongozi wa Taasisi ya Sayyid Al-Shuhadaa, kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuwahudumia Waumini na Jamii kwa ujumla. Alisema kuwa utumishi kwa watu ni miongoni mwa matendo bora zaidi kama alivyosisitiza Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).

“Hakuna jambo bora zaidi mbele ya Allah kama kumtumikia Mwanadamu na kumletea faraja. Huyu ndiye mfano wa kweli wa mja anayefuata nyayo za Mtume wetu Muhammad (saww),” alisema Sheikh Jalala.

Sheikh Hemed Jalala : “Kuwatumikia Watu ni Ibada Kubwa Zaidi” - Akihutubia Hafla ya Maulid Ngarenaro - Arusha +Picha

Aidha, Sheikh Jalala alitumia nafasi hiyo kuhimiza Amani, Upendo, na Mshikamano miongoni mwa wananchi wote, akisisitiza kuwa Maulid ya Mtume ni tukio la kiroho linalopaswa kuleta umoja, si tofauti.

“Tuendelee kuiombea nchi yetu, viongozi wetu, na hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, ili Allah ampe Hekima, Afya, na Mafanikio katika kuongoza Taifa letu,” aliongeza Sheikh Jalala.

Washiriki wa hafla hiyo walionyesha furaha kubwa kwa uwepo wa Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shi'a Ithna Ashari Tanzania na kwa ujumbe wake wa maadili, amani na upendo.

Sheikh Hemed Jalala : “Kuwatumikia Watu ni Ibada Kubwa Zaidi” - Akihutubia Hafla ya Maulid Ngarenaro - Arusha +Picha

Hafla imehitimishwa kwa Dua Maalum ya kuliombea Taifa na Jamii, sambamba na Kaswida na Mawaidha mafupi kutoka kwa vijana wa taasisi hiyo.

Your Comment

You are replying to: .
captcha