Sheikh H.Jalala: "mahusiano ya ndoa yenye mafanikio yanategemea misingi mitatu mikuu: Imani kwa Mwenyezi Mungu, Subira, na Mawasiliano ya Heshima. Bila misingi hiyo, ndoa huwa dhaifu na hukosa baraka".

11 Oktoba 2025 - 12:46

“Upendo na Maridhiano Ndiyo Nguzo Kuu ya Ndoa ya Kiislamu” | Awausia Wanandoa wapya kuishi kwa Amani na Huruma kama alivyoagiza Mtume (saww) +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C), Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, amewasili mkoani Arusha kwa ziara maalumu ya kidini, ambapo alihudhuria Ndoa Tukufu na hafla ya kijamii ya kijana wa ndugu yetu Fumbwe Salimu Mkopi, mtoto wa Mzee Salimu Mwachitogo - mmoja wa watumishi na wahudumu wa Hawzat Imam Swadiq (a.s).

“Upendo na Maridhiano Ndiyo Nguzo Kuu ya Ndoa ya Kiislamu” | Awausia Wanandoa wapya kuishi kwa Amani na Huruma kama alivyoagiza Mtume (saww) +Picha

Katika hotuba yake kwenye mnasaba huo, Sheikh Jalala aliwahimiza wanandoa wapya na jamii kwa ujumla kuishi kwa maridhiano, upendo, na heshima, akisisitiza kwamba ndoa ni mkataba mtukufu unaounganisha watu wawili kwa msingi wa dini, maadili, na huruma.

“Ndoa ni ahadi ya mbele ya Mwenyezi Mungu, si makubaliano ya kawaida. Mtume Mtukufu (s.a.w.w) amesema: "Hakuna kitu kilicho bora zaidi kwa wanandoa wawili wanaopendana kuliko ndoa". Hivyo, upendo wenu uwe kwa ajili ya Allah, si kwa matamanio ya muda mfupi,” alisema Sheikh Jalala.

“Upendo na Maridhiano Ndiyo Nguzo Kuu ya Ndoa ya Kiislamu” | Awausia Wanandoa wapya kuishi kwa Amani na Huruma kama alivyoagiza Mtume (saww) +Picha

Akinukuu maneno ya Qur’an Tukufu, Sheikh Jalala alisema:

“Na miongoni mwa Ishara Zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, naye ameweka baina yenu upendo (mawadda) na huruma...” (Surat Ar-Rum, 30:21)

Aliongeza kuwa mahusiano ya ndoa yenye mafanikio yanategemea misingi mitatu mikuu: Imani kwa Mwenyezi Mungu, Subira, na Mawasiliano ya Heshima. Bila misingi hiyo, ndoa huwa dhaifu na hukosa baraka.

“Upendo na Maridhiano Ndiyo Nguzo Kuu ya Ndoa ya Kiislamu” | Awausia Wanandoa wapya kuishi kwa Amani na Huruma kama alivyoagiza Mtume (saww) +Picha

Sheikh Jalala pia aliwakumbusha wazazi na walezi kuendelea kuwalea vijana katika misingi ya dini na maadili mema, akisema:

“Mzazi mzuri ni yule anayemlea mtoto wake ajue thamani ya ndoa, wajibu wa mwenzi, na adabu za familia. Mtume (s.a.w.w) amesema: ‘Kila mmoja wenu ni mchungaji, na kila mmoja ataulizwa juu ya kile alichokichunga.’

“Upendo na Maridhiano Ndiyo Nguzo Kuu ya Ndoa ya Kiislamu” | Awausia Wanandoa wapya kuishi kwa Amani na Huruma kama alivyoagiza Mtume (saww) +Picha

Mwisho, aliwataka wanandoa wapya kuifanya nyumba yao kuwa kituo cha upendo, ibada, na mawasiliano ya heri, na kuwa mfano wa familia za Kiislamu zinazojenga jamii yenye amani.

Your Comment

You are replying to: .
captcha