Hatua
-
Mtetemeko katika Mahusiano ya Tel Aviv na Magharibi: Biashara na Bidhaa za Makazi ya Kikoloni ya Israel Yawa Kosa
Mtandao wa Kiebrania Kan umeripoti kuongezeka kwa hatua za Norway, Uholanzi, Uingereza, Canada na Ufaransa dhidi ya biashara ya bidhaa kutoka makazi ya Israel katika Ukingo wa Magharibi, hatua zinazojumuisha marufuku ya biashara, faini, kunyang’anywa mali na vifungo vya hadi miaka 10.
-
Bashiri: Marekani haiwezi kutekeleza nia zake za kikoloni katika eneo na dunia
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema hatua za kiholela za Marekani katika eneo zinapaswa kukabiliwa kupitia sera za nchi wanachama wa BRICS, akisisitiza kuwa Washington haipaswi kufanikiwa kutekeleza nia zake mbaya katika eneo na dunia.
-
Seneta Sanders: Lazima Tumalize Sasa Hivi Vita Haramu dhidi ya Iran
Seneta Bernie Sanders amemtuhumu Donald Trump kwa kusema uongo kuhusu ahadi yake ya kumaliza vita visivyo na mwisho, na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vita dhidi ya Iran.
-
Kamanda wa IRGC: Shambulio la Kigaidi katika Harusi Kohestak Lafichua Uso Mwovu wa Marekani kwa Kuwalenga Raia Wasio na Hatia
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Meja Jenerali Ahmad Vahidi, amesema shambulio la kigaidi lililolenga sherehe ya harusi katika eneo la Kohestak nchini Iran limefichua kile alichokiita “uso mwovu na wa kishetani” wa Marekani, akisisitiza kuwa damu ya wahanga wasio na hatia haitapotea bure.
-
IRGC: Mashambulizi ya Maadui Yanafanya Kufungwa kwa Mlango wa Hormuz Kuwa Imara Zaidi
IRGC imetangaza kuanza kwa majibu dhidi ya mashambulizi ya maadui, ikisema imefanikiwa kuangusha ndege ya kisasa isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 na kwamba upinzani wa wapiganaji wake katika Mlango wa Hormuz umevuruga mipango ya viongozi wa Marekani.
-
China: Hatua za upande mmoja za Marekani dhidi ya wanaoiunga mkono Iran ni haramu
China imepinga vikali vitisho vya Marekani vya kuweka vikwazo dhidi ya nchi zinazofanya biashara na Iran, ikisisitiza kuwa hatua za upande mmoja za shinikizo na vikwazo hazina uhalali na hazisaidii kutatua mzozo.
-
Mahakama ya Israel Yasitisha Pendekezo la Ben Gvir la Kuweka Mamba Kuzunguka Gereza la Ketziot
Mahakama ya Israel imesitisha pendekezo la Waziri wa Usalama wa Taifa, Itamar Ben Gvir, la kuweka mamba kuzunguka Gereza la Ketziot linalowashikilia wafungwa wa Kipalestina, kufuatia kesi iliyowasilishwa na shirika la kutetea haki za wanyama.
-
Kuwait yafuta uraia wa Sheikh Hussein Al-Matouq na wanaharakati wengine watano
Amir wa Kuwait ametangaza kufuta uraia wa Ayatullah Sheikh Hussein Al-Matouq na wanaharakati wengine watano. Hatua hiyo imehusishwa na kesi za kiusalama, huku wakosoaji wakilaani uamuzi huo na kuuelezea kama ishara ya kuzorota kwa hali ya kisiasa nchini Kuwait.
-
Kutoka Damu ya Kiongozi Hadi Ahadi ya Umma: Tafakuri Kuhusu Falsafa ya Mwendelezo wa Muqawama
Ujumbe kati ya Hizbullah ya Lebanon na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu unaonyesha mwendelezo wa fikra ya uongozi, mradi wa Muqawama na mwanzo wa hatua mpya katika historia.
-
Marekani yaiondoa ndege yake ya upelelezi MQ-4C Triton kutoka Jordan kuelekea Italia baada ya mashambulizi ya Iran
Ripoti zinaeleza kuwa Marekani imeiondoa ndege yake ya kisasa ya upelelezi aina ya MQ-4C Triton kutoka Jordan na kuihamishia Italia, hatua inayokuja baada ya mashambulizi ya Iran dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Wanazuoni wa Bahrain Wataka Kuachiliwa Mara moja kwa Wanazuoni wa Dini Waliokamatwa
Wanazuoni wa Bahrain wametoa wito wa kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa wanazuoni wa dini waliokamatwa, wakiiwajibisha serikali ya Bahrain kwa madhara yoyote ya kimwili au kisaikolojia yatakayowapata wakiwa mahabusu.
-
Iran Yatangaza Mpango Kabambe wa Anga za Juu wa 2026, Yazindua Mradi wa Satelaiti 24 za “Shahid Soleimani”
Shirika la Anga za Juu la Iran limetangaza mipango mikubwa ya mwaka 2026, ikiwemo kuzindua satelaiti ya kwanza ya rada iliyotengenezwa nchini, kuendeleza mradi wa satelaiti 24 za “Shahid Soleimani” na kuharakisha maendeleo ya satelaiti za mawasiliano na uchunguzi wa ardhini.
-
IRGC yadai kulenga Kambi ya Anga ya Amir Hassan nchini Jordan kwa makombora na ndege zisizo na rubani
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), vikosi vyake vimedai kulenga majukwaa ya makombora, maghala ya mafuta na maeneo ya kuhifadhia silaha katika Kambi ya Anga ya Amir Hassan nchini Jordan, katika kile ilichokieleza kuwa ni hatua ya kujibu ukiukaji uliofanywa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Vyombo vya Habari vya Kiarabu Vyaupa Uzito Ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu; Vasisitiza Ulipizaji wa Damu na Kuendelea kwa Muqawama
Vyombo vya habari mashuhuri vya eneo hilo kutoka Lebanon, Iraq, Yemen, Palestina, Qatar na Saudi Arabia, vimeripoti kwa upana ujumbe wa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, uliotolewa baada ya kumalizika kwa ibada kubwa ya mazishi ya Kiongozi huyo aliyefariki akiwa shahidi. Vyombo hivyo vimeutaja ujumbe huo kuwa ni ishara ya kuanza kwa hatua mpya katika uongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Miongoni mwa mambo makuu yaliyoangaziwa katika taarifa hizo ni pamoja na kusifiwa kwa ushiriki wa kihistoria wa wananchi, uhusiano kati ya Mapinduzi ya Kiislamu na harakati ya Ashura, kuendelea kwa mbele ya Muqawama (upinzani dhidi ya dhuluma), pamoja na kusisitizwa kwa ulipizaji wa damu za mashahidi wa vita vya hivi karibuni.
-
IRGC yatangaza kufungwa kwa muda kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz baada ya tukio la meli kupuuza maonyo
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kufungwa kwa muda kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz, likisema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kile lilichodai kuwa ni ukiukaji wa maelekezo ya usalama wa baharini na kuendelea kwa uingiliaji wa mataifa ya kigeni katika eneo hilo.
-
Iran: Ukiukaji wa Ahadi za Marekani Utakabiliwa na Hatua za Kujibu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema Iran haijaomba mazungumzo na Marekani, akisisitiza kuwa sera ya Jamhuri ya Kiislamu inategemea kanuni ya "ahadi kwa ahadi" na kwamba ukiukaji wowote wa ahadi za Washington utakabiliwa na jibu la Iran.
-
Kim Jong Un Aagiza Korea Kaskazini Kuimarisha na Kupanua Uwezo wa Silaha za Nyuklia
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameagiza nchi yake kuongeza na kuimarisha uwezo wa vikosi vya nyuklia, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha uwezo wa kujilinda dhidi ya vitisho vya usalama.
-
Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi: Wageni Hawana Haki katika Mlango wa Hormuz
Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC Navy) limesema kuwa mataifa ya kigeni hayana haki yoyote katika eneo la Iran na Mlango wa Hormuz, likionya kuwa hatua za kijeshi za Marekani zinatishia usalama wa njia hiyo muhimu ya kimataifa.
-
Iran Yatangaza Kushambulia Malengo ya Kijeshi ya Marekani Nchini Qatar
Iran imetangaza kuwa imefanya mashambulizi dhidi ya malengo ya kijeshi ya Marekani yaliyoko nchini Qatar ikijibu mashambulizi ya Marekani Dhidi yake na katika hatua inayoashiria kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi kati ya Tehran na Washington.
-
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Aitaka Baraza la Usalama Kuepuka Hatua za Uchochezi
Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, amesema Baraza la Usalama linapaswa kuunga mkono diplomasia na kuepuka hatua zinazoweza kuchochea mvutano au kudhoofisha mazungumzo yanayoendelea.
-
Kiongozi wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (SAW): Vikosi vyetu vya ulinzi viko tayari kuimarisha mamlaka na usalama wa taifa
Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (SAWW), Meja Jenerali Ali Abdullahi, amesema vikosi vya ulinzi vya Iran viko katika utayari wa hali ya juu kulinda usalama wa taifa, haki za wananchi na kukabiliana na vitisho vyovyote vinavyolenga nchi hiyo.
-
Mtangazaji wa Fox News: Kusitishwa kwa Vita Kabla ya Uchaguzi wa Novemba Kumenufaisha Trump na Warepublican
Mtangazaji wa Fox News ameeleza kuwa kusitishwa kwa vita kwa muda hadi uchaguzi wa Novemba kunaweza kuwanufaisha Warepublican na kumpa Rais wa zamani Donald Trump nafasi kubwa ya kisiasa, huku akisisitiza umuhimu wa “mtazamo mpana wa maslahi ya taifa.”
-
Iran Yatangaza Uzinduzi wa AlphaZa, Dawa ya Kwanza ya Ndani ya Tiba ya Saratani kwa Teknolojia ya Mionzi ya Alpha
Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) limetangaza kuwa linakaribia kuzindua rasmi AlphaZa, dawa ya kwanza iliyotengenezwa nchini humo kwa kutumia teknolojia ya mionzi ya alpha, inayolenga kutibu saratani zilizo katika hatua za juu na zinazoshindikana kwa matibabu ya kawaida. Hatua hiyo inaashiria mafanikio makubwa ya Iran katika matumizi ya amani ya teknolojia ya nyuklia katika sekta ya afya.
-
Kundi la “Hanzala” Latuma Onyo Kali kwa Jeshi la Wanamaji la Marekani, Latishia Majibu Makali
Kundi la mtandao linalojiita “Hanzala” limetoa onyo kali kwa wanamaji wa Jeshi la Wanamaji la Marekani, likiwataka kuwasiliana na familia zao, likidai kuwa makombora yako tayari na likitahadharisha kujibu kwa nguvu iwapo kutatokea uchokozi dhidi ya Iran.
-
IRGC Yathibitisha Kushambulia Makao Makuu ya Kikosi cha Tano cha Jeshi la Wanamaji la Marekani Bahrain Kwa Kutumia Droni
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) wamedai kufanya shambulizi la ndege zisizo na rubani dhidi ya makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Jeshi la Wanamaji la Marekani nchini Bahrain, katika kile walichokiita kujibu mashambulizi dhidi ya maeneo ya kusini mwa Iran.
-
Tehran Yalaani Uchokozi wa Kijeshi wa Marekani Dhidi ya Iran, Yasisitiza Haki ya Kujilinda
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali kile ilichokiita “uchokozi wa kijeshi” wa Marekani dhidi ya nchi hiyo, ikisisitiza kuwa Iran haitasita kutumia haki yake ya kujilinda dhidi ya mashambulizi yoyote yanayoilenga.
-
Mtandao wa Israel Wakiri: Mizani ya Kimkakati Inaendelea Kubadilika kwa Faida ya Iran
Mtandao wa Channel 12 wa Israel umekiri kuwa mashambulizi ya makombora ya Iran dhidi ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yameonesha uwezo wa Tehran kuunganisha tena medani mbalimbali za mapambano, huku Israel ikikabiliwa na changamoto mpya za kimkakati.
-
Mohsen Rezaei: Mashambulizi dhidi ya Iran yamejibiwa, hatua mpya zitakabiliwa na majibu makali zaidi
Mohsen Rezaei amesema kuwa wale waliofanya mashambulizi dhidi ya Iran tayari wamepata majibu yao, akionya kuwa hatua yoyote mpya ya uchokozi itajibiwa kwa nguvu zaidi na gharama kubwa kwa wavamizi.
-
Sheikh Pro.Alhad Mussa Salum: Serikali Hupambana na Kuchukua Hatua dhidi ya Wanaotishia Maslahi Yake, Sio kwa Msingi wa Dini
Sheikh Prof.Alhad Mussa Salum: "Nchi ya Tanzania ni nchi ya Amani na sisi sote ni Watanzania, tunaishi kwa Upendo na Amani na watu wote. Uislamu ni Amani na unatufundisha kuishi kwa wema na watu wote."
-
Araghchi: Hatua Yoyote ya Uhasama Dhidi ya Iran Itajibiwa kwa Haraka na kwa Nguvu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vinafanya operesheni za kujihami kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kwamba malengo yaliyoshindikana kufikiwa kwa vikwazo na vita hayawezi kupatikana kwa kuongeza mashinikizo ya kijeshi.