Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo tarehe 30 Agosti 2025 – Jumamosi
Mtihani wa Wiki kupitia Kitengo cha Taaluma umefanyika katika Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s) - Jijini Dar-es-salaam - Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya masomo, mtihani wa kila wiki umefanyika leo ukiwashirikisha wanafunzi wa vitengo mbalimbali. Mitihani hii imeandaliwa na kufanyika kwa utaratibu maalum kwa lengo la kupima kiwango cha maendeleo ya kielimu ya wanafunzi na pia kuimarisha maandalizi yao ya kitaaluma.
Aidha, kupitia mitihani hii ya wiki, walimu hupata nafasi ya kufuatilia maendeleo ya kielimu kwa kila mwanafunzi, kutambua changamoto zinazojitokeza katika masomo, na kuweka mikakati ya kuboresha ufaulu. Hatua hii ni sehemu muhimu ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata uelewa wa kina na kuendelea kwa uthabiti katika safari yao ya kielimu na ya kidini.
Your Comment