Uongozi wa Lady Zahra Islamic Pre and Primary School umeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya elimu, kuongeza ubora wa ufundishaji pamoja na kuimarisha malezi ya watoto kwa misingi ya dini, nidhamu na maarifa ya kisasa.

7 Desemba 2025 - 14:54

Mahafali ya Pili Lady Zahra Islamic Pre and Primary School Yafanyika kwa Mafanikio Makubwa Kondoa – Dodoma +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Shule ya Awali na Msingi Lady Zahra Islamic Pre and Primary School iliyopo Kondoa, mkoani Dodoma, imefanya mahafali yake ya pili kwa mafanikio makubwa, katika tukio lililohudhuriwa na wazazi, walezi, walimu pamoja na viongozi mbalimbali wa shule.

Mahafali hayo yaliandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la awali waliokamilisha masomo yao tayari kujiunga rasmi na elimu ya msingi ndani ya shule hiyo. Wanafunzi hao wamefanikiwa kuhitimu katika mazingira ya nidhamu, maadili mema na malezi ya Kiislamu.

Mahafali ya Pili Lady Zahra Islamic Pre and Primary School Yafanyika kwa Mafanikio Makubwa Kondoa – Dodoma +Picha

Wazazi na walezi waliohudhuria hafla hiyo walijitokeza kwa wingi kuwapongeza watoto wao kwa hatua waliyofikia, huku wakieleza furaha na kuridhishwa kwao na matokeo ya juhudi za walimu pamoja na uongozi wa shule hiyo. Aidha, wazazi wamewapongeza walimu na wasimamizi wa shule kwa jitihada zao kubwa katika kuwanoa na kuwaandaa watoto hao kielimu, kiakili na kimaarifa kwa mafanikio yanayoonekana.

Kwa upande wake, uongozi wa Lady Zahra Islamic Pre and Primary School umeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya elimu, kuongeza ubora wa ufundishaji pamoja na kuimarisha malezi ya watoto kwa misingi ya dini, nidhamu na maarifa ya kisasa.

Mahafali ya Pili Lady Zahra Islamic Pre and Primary School Yafanyika kwa Mafanikio Makubwa Kondoa – Dodoma +Picha

Mahafali hayo yalipambwa na burudani mbalimbali za wanafunzi, ikiwemo mashairi, nashida, maonesho ya vipaji pamoja na dua maalumu ya kuwaombea wanafunzi hawa safari njema katika ngazi inayofuata ya elimu.

Mahafali ya Pili Lady Zahra Islamic Pre and Primary School Yafanyika kwa Mafanikio Makubwa Kondoa – Dodoma +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha