Wanafunzi
-
Spika wa Bunge la Iran: "Iran Haitaikubali Utawala wa Kigeni"
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, ameweka wazi kuwa taifa la Iran halitawahi kukubali kutawaliwa na mataifa ya kigeni na litalinda uhuru wake kwa gharama yoyote.
-
Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi:
“Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimewapiga maadui zao Kofi lisilosahaulika”
Jenerali Mousavi alisema kuwa kipindi cha masomo ya kijeshi kwa wanafunzi hao kilitokea katika wakati wa kipekee - wakati ambao muqawama ulithibitisha ushindi wa imani juu ya dhulma na ubabe wa kimataifa.
-
Taqwa na Umuhimu Wake | Ijumaa - Khutba na Sala ya Dhuhri katika Chuo cha Dini cha Wanafunzi wa Kike cha Hazrat Zainab (SA)- Kigamboni - Dar-es-salaam
Lengo Kuu la mada iliyowasilishwa ni: Kukuza roho ya ibada, kuimarisha umoja wa kijamii, na kuhimiza utamaduni wa Sala ya Ijumaa miongoni mwa wanafunzi wa dini
-
Hawzat ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni yaendelea kuhuisha Ibada ya Dua ya Nudba | Iliyojaa Mafunzo ya Subira, Imani na Mapenzi kwa Imam wa Zama (as)
Ibada hii hujenga umoja wa kiroho, maadili mema na moyo wa subira, na hivyo kufanya wiki kuanza kwa baraka na nuru ya dua.
-
Mkutano wa Wanafunzi wanaoongea Lugha ya Kiurdu Wanaokaa Mjini Qom - Iran; katika Kumbukumbu ya Mwaka wa Shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah
Hujjatul-Islam Fakhrian aliandika mada yake kwa kuanzia na nukuu ya Kiungu (alirejea aya za Quran) na kutangaza kuwa: azma ya Mwenyezi Mungu ni kuwapa walio dhaifu nafasi ya kuwa waanzilishi na warithi wa dunia; azma hiyo inatimia kwa njia moja tu — kupitia mapambano na kujitolea. Kwa hivyo, alisisitiza, hakuna njia nyingine ya kuangusha mfumo wa udikteta wa kigeni isipokuwa kupitia mapambano.
-
Darasa la Qur’an Tukufu katika Madrasat ya Mabanati ya Hazrat Zainab (sa) Laendelea kwa Mafanikio Makubwa
Darsa hili la Qur’an Tukufu linawafundisha zaidi Wanafunzi kuwa Qur'an ni mshirika na muombezi wa yeyote mwenye kushikamana nayo Siku ya Kiyama, hummulikia njia yake hapa duniani, na humuinua katika ngazi za juu Peponi
-
Mkutano wa Mwakilishi wa Kanda wa Al-Mustafa na Wanafunzi kutoka Tanzania, Burundi na Malawi katika Kituo cha Bayan
Katika mkutano huo, Hujjatul-Islam Taqavi alieleza kufurahishwa kwake na kufanyika kwa kikao hicho, na alisisitiza umuhimu wa kunufaika kikamilifu na uwezo mkubwa wa kituo hiki cha elimu. Aliwahimiza wanafunzi kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika kituo cha Bayan ili kupata maarifa na stadi muhimu kwa ajili ya maisha na kazi zao za baadaye.
-
Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam | Mtihani wa Kila Wiki: Hatua ya Kuimarisha Uelewa na Maandalizi Bora ya Kielimu na Ufaulu wa Wanafunzi
Kupitia mitihani hii ya wiki, walimu hupata nafasi ya kufuatilia maendeleo ya kielimu kwa kila mwanafunzi, kutambua changamoto zinazojitokeza katika masomo, na kuweka mikakati ya kuboresha ufaulu.
-
Mgogoro wa marufuku ya Hijabu katika mji wa “Axum” nchini Ethiopia / Wanafunzi Waislamu warejea shuleni kwa amri ya mahakama
Katika nchi yenye historia ya kuishi kwa amani baina ya dini mbalimbali, mgogoro wa hijabu katika mji wa Axum umeibua tena mjadala kuhusu uhuru wa kidini nchini Ethiopia. Uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama Kuu ya eneo la Tigray unaweza kuwa hatua muhimu katika kuthibitisha haki za Waislamu na kuimarisha msingi wa usawa wa uraia .
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu atoa rambirambi kufuatia kifo cha Msanii wa Kiirani Mahmoud Farshchian: "Ameacha nyuma kazi za sanaa zisizofutika"
"Msanii mashuhuri na maarufu, Bwana Mahmoud Farshchian, alikuwa nyota angavu katika anga ya sanaa ya Kiirani. Uaminifu wake na ucha Mungu wake vilimuwezesha kuutumia uwezo wake wa kipekee katika kuhudumia maarifa na mambo ya kidini, na ameacha nyuma kazi za sanaa zisizofutika. Rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Nawasilisha rambirambi za dhati kwa familia yake, marafiki zake, wanafunzi wake, na jamii ya wasanii nchini."
-
Mitihani ya Kila Wiki - Chuo Kikuu cha Al-Mustafa(s), Dar es Salaam - Tanzania
Mchakato huu umefanyika chini ya usimamizi makini wa walimu na uongozi wa chuo ili kuhakikisha haki, uadilifu wa kielimu na nidhamu ya kimasomo vinazingatiwa ipasavyo.
-
Mwanachama wa Baraza la Wataalam wa Uongozi katika mahojiano na Abna: Tunahitaji Hawza za Dini ambazo matokeo yake yatakuwa "Wazalishaji wa maarifa"
Mwanachama wa Baraza la Wataalam wa Uongozi alisema: Hawza ya dini inatakiwa kutafakari kwa makini kuhusu wanafunzi wake ambao hujiunga na mashirika mengine na mara nyingine hufanya kazi ambazo ni tofauti kabisa na maarifa au mafunzo yao waliyoyapokea.