Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (as) - ABNA -, Ayatollah Udhma Imam Sayyid Ali Khamenei alitoa salam za rambirambi siku ya Jumatano, tarehe 20 Agosti 2025, kufuatia kifo cha msanii maarufu wa Kiirani, Mahmoud Farshchian. Katika taarifa hiyo, alisisitiza kuwa Farshchian alikuwa “nyota angavu katika anga ya sanaa ya Kiirani.”
Nukuu kamili ya ujumbe wa Imam Khamenei:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
"Msanii mashuhuri na maarufu, Bwana Mahmoud Farshchian, alikuwa nyota angavu katika anga ya sanaa ya Kiirani.Uaminifu wake na uchamungu wake viliuwezesha uwezo wake wa kipekee kuhudumia elimu na masuala ya kidini.Ameacha nyuma kazi za sanaa zisizofutika. Rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.Nawasilisha rambirambi za dhati kwa familia yake, marafiki, wanafunzi wake, na jamii ya wasanii wa nchi yetu."
Rambirambi kwa kifo cha mwanasiasa wa Kiirani Ahmad Tavakoli
Aidha, Imam Sayyid Ali Khamenei alitoa pia salam za rambirambi kufuatia kifo cha Mwanasiasa mashuhuri Ahmad Tavakoli.
Nukuu ya ujumbe wake:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
"Nawasilisha salamu za rambirambi kwa kifo cha ndugu mpiganiaji wa imani na mkweli, Mheshimiwa Bwana Ahmad Tavakoli (Rehema ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake), kwa familia yake tukufu, marafiki na wenzake. Juhudi zake za dhati kama mpambanaji mwenye ushawishi katika Baraza la Ushauri la Kiislamu, serikalini, na taasisi nyingine za mapinduzi, hazitasahaulika miongoni mwa wale waliomfahamu. Rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake."
Your Comment