Sayyid Ali Khamenei
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameipongeza timu ya taifa ya Iran ya mieleka ya Greco-Roman kwa ushindi wao wa ubingwa wa dunia
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michezo ya nchi yetu ambapo Timu ya Taifa ya mieleka ya “freestyle” na “Greco-Roman” zimefanikiwa kwa pamoja kutwaa ubingwa wa dunia katika mashindano moja.
-
Kiongozi wa Mapinduzi Katika Mkutano na wanachama wa Serikali:
"Tuweke roho ya Kazi na Juhudi juu ya hali ya Kutokuwa Vitani wala kuwa na Amani (Hali ya 'si vita, si amani')
Ayatollah Khamenei katika kikao na Rais pamoja na Baraza la Mawaziri alisisitiza juu ya umuhimu wa 'kutawala kwa hali ya kazi, juhudi na matumaini' dhidi ya 'hali ya si vita wala amani'
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ataka Utekelezaji wa Makubaliano ya Kistratejia kati ya Iran na China
Ayatollah Khamenei amesisitiza nafasi ya kihistoria na ya kimkakati ya Iran na China katika bara la Asia na duniani, na akasema kuwa: "Iran na China, zikiwa na historia ya ustaarabu wa kale katika pande mbili za Asia, zina uwezo wa kuleta mabadiliko katika medani ya kimataifa na kikanda. Kuweka katika vitendo vipengele vyote vya makubaliano ya kistratejia, kutarahisisha njia hii."
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu atoa rambirambi kufuatia kifo cha Msanii wa Kiirani Mahmoud Farshchian: "Ameacha nyuma kazi za sanaa zisizofutika"
"Msanii mashuhuri na maarufu, Bwana Mahmoud Farshchian, alikuwa nyota angavu katika anga ya sanaa ya Kiirani. Uaminifu wake na ucha Mungu wake vilimuwezesha kuutumia uwezo wake wa kipekee katika kuhudumia maarifa na mambo ya kidini, na ameacha nyuma kazi za sanaa zisizofutika. Rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Nawasilisha rambirambi za dhati kwa familia yake, marafiki zake, wanafunzi wake, na jamii ya wasanii nchini."
-
Katika Kumbukizi ya Imam Reza (a.s): Kiongozi Mkuu Atoa Wito wa Kulinda Umoja na Kukemea Jinai za Kizayuni
Ayatollah Khamenei: "Marekani Haitaki Iran Isimame Imara, Bali Itii Amri Zake".
-
Sayyid Ali Khamenei: "Utawala wa Kizayuni haukufikiria kamwe kupokea mashambulizi kama haya kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu".
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu - Leo akihutubia Taifa la Iran, ametoa ufafanuzi mzuri mno wa matukio yalivyojiri, na kauli imara za kutia moyo kwa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambazo kwa hakika zimeonyesha mshikamano wa kitaifa, ujasiri, na kukataa kuachia madikteta au nguvu za kigeni na kibeberu kutawala na kuidhibiti Kijeshi Mashariki ya Kati. Pia, kauli za Kiongozi huyu imara na mwenye busara na hekima ya hali ya juu, zinaonyesha msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya nje, na kutotetereka katika suala zima la kuifyekelea mbali mikono ya adui yeyote yenye nia ovu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Imamu wa Ijumaa wa Baghdad: Waislamu wote wanapaswa kusimama na Ayatollah Khamenei
Imamu wa Ijumaa wa Baghdad ametoa taarifa yenye maneno makali kufuatia jinai ya hovyo ya Trump.