16 Oktoba 2025 - 00:07
Chuo cha Al-Mustafa (s) - Tanzania Kimeandaa Kongamano la Kielimu Kuhusu Ustaarabu wa Magharibi na Mikakati yake ya Kikoloni

Ustaarabu wa Magharibi na misingi ya kuuelewa ipasavyo.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Idara ya Utafiti wa Kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (s.a.w.w), Tawi la Dar-es-Salaam imeandaa Kongamano la kielimu lenye kichwa: "Hali Halisi ya Ustaarabu wa Magharibi na Mikakati yake ya Kikoloni katika Fikra za Kiongozi Mtukufu Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (H.A)".

Mada Kuu za Utafiti:

  1. Mikakati ya Magharibi, mbinu zake na sababu za udhibiti wake duniani.
  2. Mataifa ya kikoloni: Historia yake ya ukoloni na maeneo yaliyowahi kuwa chini ya utawala wake.
  3. Ustaarabu wa Magharibi na misingi ya kuuelewa ipasavyo.

Muda: Alhamisi, tarehe 16 Agosti 2025
Saa: Kuanzia 4:00 Asubuhi hadi 6:00 Mchana
Mahali: Msikiti wa Chuo Kikuu cha Jamiat Al-Mustafa(s).

Wote Mnakaribishwa Kushiriki.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha