Jamiat Al-Mustafa
-
Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa - Dar-es-salaam - Tanzania kimeandaa Kongamano la Kisayansi kuhusu Maendeleo katika Ulimwengu wa Kiislamu
Kongamano hili litajadili juu ya Maendeleo katika Ulimwengu wa Kiislamu kati ya changamoto na mkakati. Mhadhiri: Samahat Sheikh Mulaba Saleh. Siku ya: Jumamosi; 19/04/2025. Kuanzia: 10 - 12:00 AM. Katika Ukumbi wa Sala wa Chuo cha Jamiat Al- Mustafa. Watu wote mnakaribishwa kuhudhuria katika nad'wa hii ya Kisayansi.
-
Siri na Falsafa ya Ratiba ya Darsa ya "Subhi ya Kimaanawi" kwa Wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa, Dar-es-Salam, Tanzania + Picha
Maulamaa wakubwa katika historia zao, walikuwa wakitafuta Adabu (Maadili) kwanza, kisha ndio wanaitafuta elimu. Wengine walikuwa wakiitafuta adabu kwa muda wa miaka 30, na elimu wanaitafuta kwa muda wa miaka 20.
-
Kozi ya Kompyuta kwa Vitendo ya ICDL kwa Wanafunzi wa Hawzat Sayyidat Zainab (s.a) - Jamiat Al-Mustafa, Dar -es- Salaam - Tanzania
ICDL inawakilisha Leseni ya Kimataifa ya Fani ya (Computer) Kompyuta. Na hiyo ndio maana ya Kozi hii ya ICDL - Yaani: International Computer Driving License. Hii ni Kozi muhimu katika Kozi za Kompyuta ambazo zinauwezo wa kumsaidia na kumsapoti mtu yeyote kujikwamua Kiuchumi.
-
Tamasha la 30 la Kimataifa la Al-Mustafa la Qur'an na Hadithi - Zanzibar, Tanzania limefanyika kwa mafanikio makubwa
Tamasha hili la Mashindano ya Qur'an Tukufu, ni katika kuhuisha utajo wa Quran Tukufu, na hii ni harakati muhimu ya kuthamini na kuenzi Qur'an Tukufu inayoendelea nchini Tanzania, chini ya Usimamizi na Uongozi bora wa Hojjat Al-Islam Dr. Ali Taqavi (Mwenyezi Mungu Amuhifadhi) kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika uwanja Tablighi na khidma kwa Qur'an Tukufu, kwa hakika anajituma na kuhakikisha kuwa nuru ya elimu na maarifa ya Quran na ahlulbayt (as) vinazidi kuwaangazia watu wa jamii mbalimbali nchini Tanzania.