Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo Ijumaa, tarehe 8 Agosti 2025, wanafunzi wa Chuo cha Kidini cha Al-Mustafa (s) Foundation kilichopo Mbezi Beach, Jijini Dar-es-Salaam, wamehuisha usomaji wa Dua Muhimu ya Nudba kwa muda wa dakika 30.
Dua hii ni sehemu ya mazoea ya kidini yanayolenga kuimarisha ibada na kuleta msukumo wa kiroho kwa waumini.
Dua ya Nudba ni dua maarufu yenye kumbukumbu za Imamu Hussein (AS) na wafuasi wake, pamoja na maombi ya msamaha na shukrani kwa Mwenyezi Mungu (SWT).
Matukio kama haya ya Usomaji wa Dua mbali mbali yanaongeza moyo wa ibada miongoni mwa Wanafunzi na hutoa nafasi ya kuungana kiroho katika jamii ya Hawza hiyo ya Kidini, huku ukihimiza umuhimu wa Dua kama Silaha ya Waumini katika maisha yao ya kila siku.
Your Comment