Dar es salaam
-
Mfululizo wa Vikao vya Qur’ani Waendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni, Dar es Salaam
Mfululizo wa vikao vya Qur’ani umeendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni – Dar es Salaam, chini ya uongozi na ufundishaji wa Sheikh Muhammad Jaafar. Vikao hivyo vinawalenga wanafunzi wa shule hiyo na vinazingatia kukuza uelewa wa Qur’ani kupitia elimu, kuhifadhi, usomaji, tafakuri na tafsiri ya aya za Qur’ani Tukufu. Kuendeleza programu hizi kunalenga kuwajengea wanafunzi uhusiano wa karibu na Qur’ani na kuwasaidia kuelewa na kutumia mafundisho yake katika maisha yao ya kila siku.
-
Wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (s) Kushiriki Maulid ya Mtume Muhammad (saww) Temeke, Dar es Salaam
Sheikh Abbas Ramadan, Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, atoa wito kwa Waislamu kujenga umoja na mshikamano kwa kujifunza mafundisho ya undugu kutoka kwa Mtume Muhammad (saww).
-
Sheikh Abbas Ramadhan Aongoza Kikao Maalum cha Baraza la Masheikh Mkoa wa Dar es Salaam
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Abbas Ramadhan, ameongoza kikao maalum cha Baraza la Masheikh wa Mkoa kilicholenga kupitia na kuchuja majina ya wagombea wa uongozi wa Baraza la Masheikh katika ngazi ya wilaya.
-
Hafla ya Ugawaji Zawadi kwa Washindi wa Mashindano ya Uandishi wa Muhtasari "Summary Writing" Yafanyika Kigamboni - Dar-es-salaam
Katika hafla iliyofanyika katika shule ya wasichana ya Kigamboni, washindi wa mashindano ya kuandika muhtasari kuhusu “Shahada ya Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (ra)” walikabidhiwa zawadi maalum katika mwendelezo wa masomo ya Qur’an chini ya usimamizi wa Bi. Fatma Ma‘suma, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha elimu, ubunifu na ushindani wenye tija kwa wanafunzi.
-
Tanzania Yakamata Pakiti 20 za Skanka Zenye Kilogramu 20 Kwenye Bus la Kimataifa, Temeke - Dar-es-salaam
Mamlaka ya DCEA imekamatwa pakiti 20 za skanka zenye uzito wa kilo 20.03 zilizofichwa kwenye balo la mitumba ndani ya bus la Scania la King Masai Tours, lenye namba za usajili AAM 297 CA, likisafiri kati ya Nampula, Msumbiji na Dar es Salaam. Watuhumiwa waliokamatwa ni Amasha Iddi Mrisho (40) kutoka Dar es Salaam na Seleman Juma Ally (32) raia wa Msumbiji. Uchunguzi na kesi za kiutumishi zinaendelea.
-
Majlis ya Kuhuisha Shahada ya Sayyidat Fatima Al-Zahra (sa) kwa Akina Mama Jijini Dar es Salaam +Picha
Katika khutba yake, Sheikh Ja'far Mwazoa alieleza kwa ufafanuzi wa kina fadhila zake nyingi, akibainisha namna ambavyo Bibi Fatima (sa) ni kigezo bora cha kuigwa na wanawake wote wa Kiislamu, na hata wanaume wa Umma wa Mtume Muhammad (saww), kutokana na uchamungu wake, hekima yake, na msimamo wake thabiti katika kutetea ukweli.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mkutano wa 32 wa Kitaifa wa Sala
Ayatollah Khamenei katika ujumbe wake kwa Mkutano wa 32 wa Kitaifa wa Sala alielezea mambo muhimu yanayohusu mkutano huu pamoja na sifa za sala.
-
Kuzingatia Umuhimu wa Swala ya Ijumaa na Tabia Njema katika Hawzat ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a) - Tanzania
Hadithi: “إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ مَکَارِمَ الأَخْلَاقِ.” “Mimi nimetumwa ili nikamilishe tabia njema.” Aya Tukufu: «قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا» (Surat Ash-Shams, Aya 9–10). "Amefaulu yule aliyeitakasa nafsi yake, na ameharibikiwa yule aliyeichafua (aliyeifisidi)".
-
Mazoezi ni Afya: Jamiat Al-Mustafa (s) Yaendeleza Michezo kwa Ajili ya Kuimarisha Afya ya Mwili na Akili
Kwa hakika, michezo na mazoezi haya yamekuwa kielelezo cha namna Uislamu unavyopenda mwili wenye nguvu, akili timamu, na mshikamano wa kijamii, ili kumsaidia Muislamu kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya kidini, kijamii na kiulimwengu.