Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Majlis maalumu ya akina mama ilifanyika Jijini Dar es Salaam ikiongozwa na Sheikh Ja’far Mwazoa, ambaye alitoa mawaidha yenye kugusa nyoyo kuhusu kifo cha kishahidi cha binti kipenzi wa Mtume Muhammad (saww), Sayyidat Fatima Al-Zahra (sa).
Katika khutba yake, Sheikh Ja'far Mwazoa alieleza kwa ufafanuzi wa kina fadhila zake nyingi, akibainisha namna ambavyo Bibi Fatima (sa) ni kigezo bora cha kuigwa na wanawake wote wa Kiislamu, na hata wanaume wa Umma wa Mtume Muhammad (saww), kutokana na uchamungu wake, hekima yake, na msimamo wake thabiti katika kutetea ukweli.
Majlis hii iliendeshwa kwa utulivu mkubwa, huku waumini wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam wakikusanyika ndani ya Ukumbi wa Husseiniyyah kwa lengo la kusikiliza mawaidha mema yanayohusu maisha, tabia, na utukufu wa Sayyidat Fatima Al-Zahra (sa).
Mkusanyiko huu uliakisi mapenzi na heshima ya waumini kwa Bibi huyu mtukufu ambaye ni taa ya uongofu kwa vizazi vyote.
Dua:
Ewe Mwenyezi Mungu, tujaalie tuuige maadili na nuru ya Sayyidat Fatima (sa),
na uwalani wale wote waliomdhulumu na kumtesa kipenzi cha Mtume wetu Muhammad (saww).

Your Comment