Msiba wa Bibi Fatima (sa) ni miongoni mwa misiba mikubwa zaidi katika historia ya Uislamu.Msiba huu unafichua watu waliopotoka na kusimama dhidi ya haki.

24 Novemba 2025 - 18:31

Malawi | Maadhimisho ya Shahada ya Bibi Fatima Zahra (sa) Yafanyika katika Shule (Hawzah) ya Al-Imam Al-Hadi (as) +Picha

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Leo, Tarehe 24-11-2025, Marasimu ya kuadhimisha kumbukumbu ya Shahada ya Bibi Fatima Zahra (SA) imefanyika katika Shule (Hawzah) ya Al-Imam Al-Hadi (as) Nchini Malawi ikihudhuriwa a wanafunzi, wazazi na waumini Wafuasi Mtume Muhammad (saww) na Aali zake Watoharifu.

Malawi | Maadhimisho ya Shahada ya Bibi Fatima Zahra (sa) Yafanyika katika Shule (Hawzah) ya Al-Imam Al-Hadi (as) +Picha

Mawaidha ya Sheikh Abdulrashid Yusuf

  1. Msiba wa Bibi Fatima (sa) ni miongoni mwa misiba mikubwa zaidi katika historia ya Uislamu.
  2. Msiba huu unafichua watu waliopotoka na kusimama dhidi ya haki.
  3. Shambulio la nyumba ya Bibi Fatima (sa) lilikuwa kosa kubwa kwa sababu:
    • Nyumba yake ilikuwa nyumba ya malaika.
    • Ilikuwa nyumba ya nuru na malezi ya maimamu, kama Imam Hasan (as) na Imam Hussein (as).
    • Ilikuwa nyumba ya baraka na mahali pa ibada pa Bibi Fatima (sa).

      Malawi | Maadhimisho ya Shahada ya Bibi Fatima Zahra (sa) Yafanyika katika Shule (Hawzah) ya Al-Imam Al-Hadi (as) +Picha

Mawaidha ya Sheikh Abdulrahman Kachara

  1. Alinukuu hadithi: Kumdhuru Fatima (sa) ni kama kumdhuru Mtume Muhammad (saww)”
    Hadithi hii ina maana nzito kuhusiana na hadhi na utukufu wa Bibi Fatima (sa).

  2. Hadithi nyingine: “Hana dini yule asiye na akili.”
    Sheikh alisisitiza kuwa kama Waislamu wangetumia akili zao ipasavyo, wangeutambua Uislamu wa kweli na wa Haki na kuufuata na kushikamana nao.

    Malawi | Maadhimisho ya Shahada ya Bibi Fatima Zahra (sa) Yafanyika katika Shule (Hawzah) ya Al-Imam Al-Hadi (as) +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha