Hujjatul Islam Taqavi, katika Hotuba yake aligusia fursa, changamoto na mikakati ya kukabiliana nazo katika nyanja za elimu, utafiti na utamaduni, na kusisitiza umuhimu wa kupanga kwa umakini na ufanisi.

Shirika Ia Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Jamiat Al-Mustafa (s) - Tanzania, Dar-es-salaam imeandaa warsha ya siku mbili iliyoratibiwa kwa ajili ya wakuu na wasimamizi wa elimu, utamaduni na utafiti wa shule zinazohusiana na zinazosimamiwa katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Zanzibar. Warsha hii ilijikita katika masuala ya kielimu, kiutafiti na kitamaduni, ikiwa na lengo la kuboresha ubora wa shughuli za shule husika.

Mwanzoni mwa kikao, Hujjatul-Islam Taqavi alitoa maelezo kuhusu malengo ya msingi ya warsha na kusisitiza mambo yafuatayo:
1_Kutumia ipasavyo uwezo na rasilimali zilizopo katika shule
2_Kukusanya, kuratibu na kusasisha taarifa za elimu, utafiti, utamaduni na Qur’ani
3_Kufanya tathmini ya changamoto za malezi na mafunzo, na kubaini maeneo yenye mapungufu
4_Kuimarisha uratibu na ushirikiano baina ya shule zinazohusiana na zinazosimamiwa katika nchi mbalimbali
5_Kuunganisha, kusawazisha na kuboresha maudhui ya mitaala na masomo
Aidha, aligusia fursa, changamoto na mikakati ya kukabiliana nazo katika nyanja za elimu, utafiti na utamaduni, na kusisitiza umuhimu wa kupanga kwa umakini na ufanisi.

Katika sehemu ya mwisho ya kikao, wakuu wa shule walitoa maoni, mitazamo na uzoefu wao, na wakawasilisha mapendekezo ya vitendo kwa ajili ya kuboresha mchakato wa elimu na shughuli za kitamaduni katika shule zao.

Your Comment