Wanawake katika jamii za Kiislamu wanachukua jukumu muhimu katika kuadhimisha kifo cha Kishahidi cha Imam Sadiq (a.s), ambapo si tu wanahudhuria kimwili katika vikao kama hivi vya Maombolezo, bali pia wanashiriki kikamilifu kwa njia ya vitendo katika kueneza mafundisho ya Imam Sadiq (as) katika nyanja mbalimbali.
Maulana Sheikh Hemed Jalala: "Adui Ibn Muljim (laana iwe juu yake), aliyempiga Imam Ali (a.s) kwa upanga wenye sumu kali, alijua kuwa hawezi kupambana na Imam Ali (a.s) akiwa nje ya Msikiti, hivyo akaona mbinu aliyokuwa nayo ni kumuwinda akiwa katika ibada (swala), kwani awapo katika swala huwa mwili wake na hisia zake zinatoweka Duniani, na anazungumza na Mola wake Mtukufu kama vile hayupo Duniani".