Mabinti
-
Dua ya Nudba Yafanyika Leo hii Ijumaa Katika Hawza ya Mabanati ya Hazrat Zainab (sa), Kigamboni - Dar-es-Salam
Usomaji wa Dua wa namna hii kawaida huvutia ushiriki mkubwa wa Wanafunzi na Wapenzi wa Ibada na Dua, na kuleta hali ya utulivu wa kiibada katika mazingira ya Chuo hiki cha Kiislamu.
-
Dua ya Nudba Yasomwa kwa Hisia Kuu na Mabinti wa Madrasa ya Hazrat Zainab (SA) Kigamboni – Wakiadhimisha Mapenzi kwa Imam wa Zama (a.t.f.s)
"Dua ya Nudba ni kilio cha roho inayotamani haki irejee. Ni kilio cha wale waliomsubiri Imam wao wa Zama kwa subira na msimamo."
-
Mabanati wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni, Dar-es-salaam, Wapatiwa Vyeti vya (ICDL) Baada ya Kukamilisha Kozi hiyo ya Mafunzo ya Kompyuta
Tunawapongeza waalimu waliowafundisha wasichana hawa wa Kiislamu kwa bidii na uaminifu, na pia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Jamiatul Mustafa (s) - Tanzania, Hojjatul Wal Muslimin, Dr.Ali Taqavi aliyekuja na wazo hili muhimu na kulisimamia kwa hekima na juhudi kubwa.
-
Heshima ya Mwanamke wa Kiislamu Katika Muonekano wa Vazi la Hijabu: Mfano wa Mabinti wa Hawzat Hazrat Zainab (sa), Dar es Salaam – Tanzania
Leo hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam - Tanzania, palifanyika Kongamano Tukufu la Qur’an ambapo wanafunzi wa kike kutoka Hawzat Hazrat Zainab (sa) walishiriki kwa umahiri na adabu kubwa. Walikuwa mfano halisi wa utekelezaji wa mafundisho bora ya Kiislamu kuhusu namna ya kujisitiri, kuishi, na kuwasilisha ujumbe wa dini kwa vitendo.
-
Kisomo cha Dua ya Kumail katika Hawza ya Hazrat Zainab (sa) – Kigamboni, Dar-es-Salaam
Hawza ya Hazrat Zainab (sa) iliyoko Kigamboni, Dar-es-Salaam, ni chuo makhsusi kwa ajili ya kuwalea mabinti wa Kiislamu kielimu na kimaadili. Chuo hiki kipo chini ya usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s) – Tanzania, na mbali na masomo ya kielimu yanayotolewa humo, wanafunzi pia hupatiwa malezi ya kiroho kwa kupitia mafundisho ya dua na ibada.
-
Hawzat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Dar-es-salaam | Wanawake katika Kuadhimisha Shahadat ya Imam Sadiq (a.s) + Picha
Wanawake katika jamii za Kiislamu wanachukua jukumu muhimu katika kuadhimisha kifo cha Kishahidi cha Imam Sadiq (a.s), ambapo si tu wanahudhuria kimwili katika vikao kama hivi vya Maombolezo, bali pia wanashiriki kikamilifu kwa njia ya vitendo katika kueneza mafundisho ya Imam Sadiq (as) katika nyanja mbalimbali.