4 Oktoba 2025 - 15:46
Kuzingatia Umuhimu wa Swala ya Ijumaa na Tabia Njema katika Hawzat ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a) - Tanzania

Hadithi: “إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ مَکَارِمَ الأَخْلَاقِ.” “Mimi nimetumwa ili nikamilishe tabia njema.” Aya Tukufu: «قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا» (Surat Ash-Shams, Aya 9–10). "Amefaulu yule aliyeitakasa nafsi yake, na ameharibikiwa yule aliyeichafua (aliyeifisidi)".

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Siku ya Ijumaa, tarehe 10 Rabiul Thani 1447AH iliyosadifiana na tarehe 3 Oktoba 2025, kikao cha kila wiki cha kidini kimefanyika katika Shule (Hawzat) ya Mabinti ya Hazrat Zainab (Salamullahi Alayha) iliyoko Kigamboni, Jijini Dar es Salaam - Tanzania.

Katika Kikao hicho cha kielimu na Maarifa ya Kidini, kilichohudhuriwa na Wanafunzi, Walimu na Viongozi wa Shule, mada kuhusu umuhimu wa Swala ya Ijumaa na nafasi yake katika kuamsha imani na kuimarisha umoja wa jamii ya Kiislamu iliwasilishwa.

Kuzingatia Umuhimu wa Swala ya Ijumaa na Tabia Njema katika Hawzat ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a) - Tanzania


Samahat Sayyid Wajih - Mzungumzaji wa kikao hicho alielezea athari kubwa ya Swala ya Ijumaa katika kuirekebisha nafsi na jamii, na kusisitiza umuhimu wa kushiriki kwa ufahamu na kwa nidhamu katika ibada hii tukufu ya Mwenyezi Mungu.

Katika sehemu ya pili ya mazungumzo yake, alizungumzia kuhusu tabia njema (husnul khuluq) kama moja ya alama za imani ya kweli, akisema:


“Tabia njema kwa watu, maneno laini na moyo wenye huruma ni funguo za mioyo ya wanadamu. Jamii ambayo wanajamii wake wanaishi kwa tabia njema, hujipatia rehema za Mwenyezi Mungu.”

Hadithi mbalimbali zilisomwa katika muktadha wa tabia Njema, na kusisitiza kumuiga Mtume Muhammad (saww) katika tabia Njema, Kwa kuwa yeye ametumwa kuja kuikamilisha na kuitimiliza tabia Njema, kama alivyosema katika Hadithi Sahihi Ifuatayo:
Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.) amesema:

Hadithi:


“إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ مَکَارِمَ الأَخْلَاقِ.”


"Mimi nimetumwa ili nikamilishe tabia njema.”

Aya Tukufu:


«قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا * وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا»


(Surat Ash-Shams, Aya 9–10).


"Amefaulu yule aliyeitakasa nafsi yake * na ameharibikiwa yule aliyeichafua (amepita patupu yule aliyeifisidi)".

Kuzingatia Umuhimu wa Swala ya Ijumaa na Tabia Njema katika Hawzat ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a) - Tanzania

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha